The House of Favourite Newspapers

Makamu wa Rais Dkt. Mpango Aweka Jiwe la Msingi Ujenzi Wa Reli Ya Kisasa NBC Yashiriki

0
Makamu wa Rais Dk Phillip Mpango akisikiliza maelezo ya ushiriki wa benki ya NBC katika ujenzi wa Reli ya kisasa(SGR) kutoka kwa Meneja wa benki ya NBC Tawi la Kahama. Simon Ntwale. wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa kipande cha nne kutoka Tabora hadi Isaka mkoani Shinyanga uliofanyika eneo la Isaka.

Katika kufanikisha miradi mbalimbali ya kimkakati Benki ya Taifa  Biashara  ya Taifa  (NBC) imetoa ahadi ya  kuwa mstari wa mbele kwenye kutoa ushirikiano kwa Serikali na Wakandarasi ili kuhakikisha miradi inayojengwa kwa manufaa ya Watanzania inakamilika kwa wakati.

Wafanyakazi wa NBC wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa ujenzi wa kipande cha nne kutoka Tabora hadi Isaka mkoani Shinyanga uliofanyika eneo la Isaka.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa pamoja na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa pamoja na viongozi wengine wa Chama na Serikali akiweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) Kipande cha nne Tabora – Isaka yenye urefu wa Kilometa 165 katika hafla iliofanyika Isaka Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akihutubia wakati wa hafla hiyo  ameitaka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Bodi ya Wakurugenzi na Wafanyakazi wa TRC kuendelea kutimiza wajibu wao wa kusimamia vizuri utekelezaji wa miradi ya kimkakati ili iweze kukamilika kwa wakati na ubora unaotakiwa.Aidha ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuwakamata wanaohujumu mradi wa Reli ya kisasa ya SGR.

“Naviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kubaini mtandao wa wizi kwenye mradi wa SGR kuwakamata wote na kuwachukulia hatua kali za kisheria” amesema Dk Mpango.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji  wa  benki ya NBC Bw. Simon Ntwale amemweleza DK Mpango namna benki hiyo inavyoshiriki kikamilifu katika ujenzi huo wa mradi mkubwa, wakati alipotembelea banda la benki hiyo.

“Sisi benki ya NBC tumeshiriki kikamilifu katika kumuwezesha mkandarasi Yapi Merkezi kununua mitambo ya kufanyia ujenzi huo pia tumewezesha zoezi la ulipaji fidia kwa wanaopitwa na mradi huu” amesema Ntwale.

Akaongeza kuwa kwa upande mwingine wamewezesha ununuzi wa vichwa na mabehewa ya kisasa kwa ajili ya mradi huo.

Awali akitoa taarifa za Ujenzi wa Mradi huo Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania Masanja Kadogosa amesema uwezo wa kubeba mizigo kupitia reli ya kisasa utakua ni tani 120 kwa behewa ikiwa ni mara tatu ya reli ya sasa yenye uwezo wa kubeba tani 40 kwa behewa.

Aidha amesema kupitia ujenzi huo,TRC inatarajia kuboresha chuo cha reli kilichopo Tabora na kuweza kutoa shahada ya uandisi katika reli mara baada ya kukamilika.

Vilevile amesema TRC imeendelea kuokoa gharama kwa kiasi kikubwa kupitia mikataba ya ujenzi wa reli ambayo hairuhusu ongezeko la gharama kutoka kwa mkandarasi kutokana na mabadiliko ya bei za vifaa na malighafi.

Leave A Reply