The House of Favourite Newspapers

MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI KAMALA HARRIS AHITIMISHA ZIARA YAKE TANZANIA-(VIDEO+PICHA)

0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango kiwa na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango akimuaga Makamu wa Rais wa Marekani Kamala HarrisĀ  na Mumewe Douglas Emhoff katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam leo tarehe 31 Machi 2023 mara baada ya kuhitimisha ziara nchini Tanzania.
Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris akiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango wakati akiwaaga wananchi mbalimbali waliojitokeza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam mara baada ya kuhitimisha ziara yake nchini Tanzania leo tarehe 31 Machi 2023.

MAKAMU wa Rais wa Marekani, Kamala Harris leo Machi 31, 2023 amekamilisha ziara yake ya kikazi nchini Tanzania na kuelekea Zambia ambako atahitimisha ziara yake barani Afrika.

Akiwa Tanzania amekutana na mwenyeji wake, Rais wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan, Ikulu Dar es Salaam na kuzungumza mambo mbalimbali ikiwepo kuimarisha ushirikiano wa mataifa haya mawili na masuala ya kiuchumi.

Pia, viongozi hao wamezungumza namna Tanzania inavyofanya vizuri kuimarisha demokrasia, na kuinua wanawake kiuchumi ambapo Kamala amempongeza Rais Samia kwa hatua mbalimbali alizochukua ikiwemo kuruhusu mikutano ya hadhara na kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari.

Kamala amekuwa na takribani wiki moja ya ziara ya kikazi barani Afrika ambapo ziara yake ilianzia Ghana.

Leave A Reply