The House of Favourite Newspapers

MAKONDA AANZA UTEKELEZAJI AGIZO LA RAIS MAGUFULI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akifuatilia taratibu za ujenzi wa Barabara ya kutokea Makao Makuu ya BAKWATA kupitia eneo la Kinondoni Shamba hadi Biafra.

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameanza kufanyia kazi agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli la kufuatilia taratibu za ujenzi wa Barabara ya kutokea Makao Makuu ya BAKWATA kupitia eneo la Kinondoni Shamba hadi Biafra.

Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini na Majini (TARURA) Kinondoni, Leopold Runji akimwelezea jambo Makonda.

Makonda amefanya ziara ya ukaguzi na kubaini nyumba nyingi kwenye eneo hilo zimejengwa kwenye hifadhi ya barabara na baadhi ya watu tayari wamelipwa fidia ambapo amewataka wananchi kushirikiana na Wakala wa Barabara Vijijini na Majini (TARURA) kuhakikisha ujenzi wa barabara unaanza mara moja.

 

Aidha ameagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), DAWASCO na TTCL kushirikiana kwa karibu na TARURA kuondoa miundombinu yao ili kasi ya ujenzi uanze.

 

Kwa upande wake Meneja wa TARURA Kinondoni, Leopold Runji amesema tayari wameanza utekelezaji wa maagizo waliyopatiwa na watahakikisha ujenzi unaenda kwa kasi na kukamilika kwa wakati.

Comments are closed.