The House of Favourite Newspapers

MAKONDA Atinga Vazi Maalum la Kuishangilia STARS – Video

MKUU  wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amewataka Watanzania kwa kushirikiana na wadau wa michezo na serikali ya awamu ya tano kutoa hamasa kwa wachezaji wa Taifa Stars ili kufanikisha timu hiyo kucheza kwa weledi na kurejea nchini ikiwa na ushindi.

 

Katika kuonyesha msisitizo, amezindua vazi maalum kwa ajili ya kuishangilia timu hiyo na kuongeza kuwa Jumamosi ya Juni 22 mwaka huu ni siku ya taifa kufanya maombi kwa ajili ya Taifa Stars ambayo itakuwa ikishuka dimbani Jumapili ya Juni 23.

 

Awali,  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo,  Dkt.  Harrison Mwakyembe, amewaomba Watanzania timu hiyo ambayo ipo kambini Misri ikijiandaa na michuano ya AFCON itakayoanza Juni 21 mwaka huu nchini Misri.

 

CHEKI RC MAKONDA Alivyotinga Vazi Maalum la Kuishangilia TAIFA STARS

Comments are closed.