The House of Favourite Newspapers

Alichokisema Alikiba Baada ya Kukutana na Balozi wa Ufaransa

MSANII wa Bongofleva, Alikiba, amefanya mazungumzo na Balozi wa Ufaransa nchini, Frederic Clavier,  leo Juni 17, 2019, ambapo wamekubaliana mambo mbalimbali ikiwemo kuendelea kubadilishana utamaduni.

 

Alikiba amethibitisha mchongo huo leo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instgram ambapo ameandika, ”Mapema asubuhi ya leo nilipata fursa ya kufanya mazungumzo na Balozi wa Ufaransa nchini – His excellence Frederic Clavier ofisini kwake”.

Akiweka wazi mazungumzo yao, amefunguka haya, ”Tumezungumza mengi kuhusu namna gani tunaweza kujenga daraja la kubadilishana utamaduni baina ya Tanzania na Ufaransa”.

 

Alikiba ni miongoni mwa wasanii ambao huenda wakawa wanafahamu kidogo lugha ya Kifaransa ambapo amewahi kuimba baadhi ya mashairi yake kwa Kifaransa katika wimbo wake wa Aje.

Comments are closed.