Makonda Ampa Gari Jingine Mwalimu Adella Aliyetapeliwa
Mwalimu Adella atoa shukrani kwa CCM na Rais Samia akisema hakika ni Chama kinachosimama Haki.
> Ampa jina Mwenezi Makonda kwa kumuita Mtetezi wa Wanyonge.
“Siku ya Novemba 9, 2023 Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Paul Makonda alipokuwa ziarani Mkoani Kagera Wilayani Bukoba Mjini alikutana na Mwalimu Adella aliyewasilisha changamoto yake kwenye Mkutano wa Hadhara ya kudhulumiwa gari lake ambalo ndio alikuwa ametoka kulichukulia mkopo na kwa muda mrefu katika kuifatilia ile gari alishindwa kuipata na mwisho wa siku ilikaa sana katika kituo cha polisi cha pale Bukoba hadi ikaharibika”
“Kiubinadamu kabisa Mwenezi Makonda aliamua kutoa gari nyingine mpya ambayo kithamani inalingana na ile gari aliyokuwa amedhulimiwa Mwalimu Adella na leo ikiwa zimepita siku sita tangu kutolewa kwa ahadi hiyo, kwa niaba ya Katibu wa NEC – Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu Paul Makonda namkabidhi Mwalimu Adela funguo , kadi na gari lenyewe ikiwa ni ukamilishaji wa ahadi iliyotolewa”
Alisema Ndg. Shaibu Akwilombe
Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa.
Naye Mwalimu adella ametoa shukrani zake kwa Mwenezi Makonda kwa kumpa jina la Mtetezi wa Wanyonge.
Aidha, Amekishukuru Chama Cha Mapinduzi kikiongozwa na Mwenyekiti wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan , kwani CCM imeonesha ni sauti inayosimama katika Haki.