The House of Favourite Newspapers

Zaidi Ya Bilioni 1.4 Yajenga Ofisi Ya Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Mara, Sagini Atoa Neno

0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini (Mb) (Kushoto), akikagua Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara linalojengwa katika eneo la Manispaa ya Musoma wenye thamani ya shilingi Bilioni 1.4 leo Novemba 17, 2023.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi (Mb) Jumanne Sagini amefanya ziara ya kutembelea na kukagua Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara katika eneo la Manispaa ya Musoma wenye thamani ya shilingi Bilioni 1.4.

Akizungumza baada ya kukagua wa Mradi huo Sagini amesema kuwa, kukamilika kwa Mradi huo utaipa heshima na hadhi Ofisi ya Kamanda wa Polisi kwani kila Kitengo kitakuwa na Ofisi yake tofauti na ilivyo kuwa sasa.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini (Mb) (Wa pili kushoto), Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara ACP Salim Morcase (Wa pili kulia), pamoja na Maafisa wengine wa Jeshi hilo kwenye picha ya Pamoja baada ya kukagua Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara linalojengwa katika eneo la Manispaa ya Musoma wenye thamani ya shilingi Bilioni 1.4 leo Novemba 17, 2023.

“Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni sikivu na nimearifiwa kuwa, fedha za awamu ya pili na tatu tayari zimetoka hivyo basi nimuombe mkandarasi kukamilisha ujenzi kama inavyoelekeza ili ofisi ianze kutumika.” Alisema

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara ACP Salim Morcase, amemshukuru Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Wizara kwa ufuatiliaji wa karibu wa Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara.

Muonekano wa Jengo la Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara linalojengwa katika eneo la Manispaa ya Musoma lenye thamani ya shilingi Bilioni 1.4 Novemba 17, 2023.

“Sisi kama Jeshi la Polisi kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchi tunatoa shukurani zetu za dhati kwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na kwako kwa ufuatiliaji wa karibu wa Mradi wa Ujenzi wa Jengo letu”. Alisema ACP Morcase

Aidha, amebainisha kuwa, Mradi huo mpaka sasa umefikia asilimia 92 na ulianza kutekelezwa Novemba 18, 2021 na unakadiriwa kumalizika mwishoni mwa mwezi Disemba mwaka 2023.

Leave A Reply