The House of Favourite Newspapers

Makonda Atua Kwenye Machinjio ya Vingunguti, Atoa Maagizo – Video

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amemtaka Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbi la moto, kuboresha miundombinu barabara inayopita maeneo ya machinjio ya Vingunguti pamoja na kuunganisha reli ili kurahisisha usafirishaji wa nyama.

 

Akizungumza leo Jumapili, Septemba 29, 2019 wakati akifanya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa machinjio ya Vingunguti Paul Makonda amesema kuwa barabara hiyo itapunguza msongamano ikiwa ni pamoja na kurahisisha usafirishaji wa nyama.

 

Aidha amemtaka Meya huyo kuangalia uwezekano wa kupanua eneo hilo la Machinjio kwa kuwalipa fidia wakazi wa maeneo yaliyozunguka machinjio.

 

Akizungumzia kuhusiana na kufurahishwa na maendeleo ya mradi huo Paul Makonda amesema. Kwa upande wake Meya Kumbilamoto amesema kuwa ameyapokea maagizo yaliyotolewa na MKuu wa Mkoa na kwamba mipango yote iliyotolewa na mkuu wa mkoa ataifanyia kazi.

 

Nae Mhandisi wa Mradi huo Mhandisi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Elisante Ulomi Amesema kuwa mradi huo unaendelea vizuri na kwamba mpaka Tarehe 20 Novemba watakuwawamekwisha.

Comments are closed.