The House of Favourite Newspapers

Makonda Awajibu Wanaomtuhumu Mkewe

Mke wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda (kulia) akiwa na rafiki yake

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewajibu wote wanaosema katika mitandao ya kijamii, kuwa mkewe si raia halali wa Tanzania na kusema kuwa, hata kila siku wataamka na kisa kipya yeye bado ataendelea kupambana na kuhakikisha Dar es Salaam inakuwa safi.

Mke wa Paul Makonda

Makonda ameyasema hayo alipokuwa ibadani katika kanisa la kiinjili la kilutheli KKKT Ushirikia wa Kimara ambapo alisema baada ya kuona wameshindwa kwa tuhuma hizi sasa wanaibua tuhuma zingine.

Paul Makonda na Mkewe

Aidha Makonda alisema kuwa anamfahamu historia ya vita dhidi ya madawa ya kulevya ya kuwa hakuna mtu aliyetoka salama. Wote walioanzisha mapambano haya hawakutoka salama, wengi waliuwawa, wengine walifungwa na wengine walipata matatizo mbalimbali sababu wahusika wa biashara hii ni watu wenye nguvu.

Salum Milongo/GPL

Comments are closed.