The House of Favourite Newspapers

Makonda: Mafanikio Vita Dhidi ya Madawa ya Kulevya Yaonekana

Makonda (kushoto) na Kamanda Siro

MKUU  wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema kelele zinazoendelea dhidi yake ni dalili za mafanikio katika vita dhidi ya dawa za kulevya.

Makonda ameyasema hayo jana alipokuwa mgeni rasmi katika tamasha la Twendezetu Kigamboni lililofanyika Kigamboni jijini Dar es Salaam ambako alisisitiza kwamba mapambano dhidi ya dawa za kulevya ni vita vya ya kufa au kupona.

Waziri Mkuu Majaliwa wa kwanza (kushoto) Paul Makonda na kamanda Siro

“Mfahamu kuwa tunapambana kati ya mauti na uzima, kelele na mwangwi unaoendelea sasa ni dalili njema kwamba tunaendelea kunyooka,” amesema Makonda.

Makonda alisema Dar es Salaam ya sasa anaifananisha na chuma kilichopinda na sasa kiko katika hatua ya kunyooka hivyo lazima zitokee kelele nyingi kama ambavyo zinaendelea sasa.

“Huwezi kufanya kazi ya kunyoosha chuma bila kusikia mwangi, kelele na maumivu kwa sababu kazi ya kukomboa vijana dhidi ya dawa za kulevya si rahisi,” alisema Makonda.

Tamasha hilo lilihudhuriwa na vingozi wengine wa serikali akiwemo  Mbunge wa Jimbo hilo, Dk Faustine Ndungulile, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Rahel Mhando na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo.

SHINDA NYUMBA AWAMU YA PILI YATIKISA JIJI LA DAR ES SALAAM

Salum Milongo/GPL

Comments are closed.