The House of Favourite Newspapers

Makonda; Wakurugenzi Wanaomchonganisha Rais Samia Na Wananchi Hatutawavumilia

0
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda amesema Chama Cha Mapinduzi hakitafumbia macho Wakurugenzi wala Kiongozi yeyete atakayejaribu ama kubainika anakuwa sehemu ya uchonganishi wa Wananchi na Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan basi CCM haitasita kumchukulia hatua kali dhidi yake.

Makonda ameyasema hayo Januari 20, 2024 alipopokea malalamiko ya mfanyabiashara wa vifaa vya ujenzi aliyetoa vifaa vyenye thamani ya Tsh Milioni 34 kwa ujenzi wa Kituo cha Afya Madanga na tangu mwezi februari mwaka 2022 hajalipwa fedha zake kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmshauri ya Pangani Bw. Isaya Mbenje , Aidha anadai Tsh Milioni 27 ambapo aliwezesha vifaa vya zoezi la usafi wa Mazingira.

Mara baada ya kupokea malalamiko hayo, Mwenezi Makonda alimtaka Mkurugenzi huyo wa Halmashauri ya Pangani Bw. Isaya kutoa majibu ya madai hayo ambapo hayakuwa majibu ya kuridhisha.

Badaa ya kusikiliza kwa makini, Mwenezi Makonda alitoa maagizo kwa Mkuu wa Wilaya ya Pangani kuhakikisha hadi kufika Jumatatu tarehe 20 Januari, 2024 Mkurugenzi awe amelipa fedha zote anazodaiwa na Mfanyabiashara huyo na iwapo malipo hayp hayatalipwa basi CCM itachukua hatua kali dhidi yao kwa kuwaondoa, ambapo amemsisitiza pia Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Kindamba kusimamia hilo.

Leave A Reply