The House of Favourite Newspapers

Makonda: Waziri Atakayefikisha Robo Mwaka Bila Ripoti Ya Kazi Atachukuliwa Hatua – Video

0

KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi, Paul Makonda amesema kutokana na Serikali kutenga Bajeti ya miradi ya Maendeleo kwaajili ya Wananchi, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinawataka Mawaziri kuwasilisha Ripoti ya kazi zao katika Sekretarieti yake

Akiongea leo Dodoma amesema “Kutokana na msingi wa Dkt. Samia kuweka bajeti kubwa ya kuwapigania na kuwaletea maendeleo Wananchi, Chama kinawataka Mawaziri wote kila robo ya mwaka ya kibajeti kuandaa taarifa na kuiwasilisha kwenye Sekretarieti ya Chama Taifa ikielezea utekelezaji wa kazi waliyopewa na Serikali”

“Kazi hii wamepewa na Mwenyekiti wetu wa Chama, Chama kinataka kupata ripoti kila robo ya Chama wamefanya nini? na Waziri yeyote atakayekaa zaidi ya Robo Mwaka (Miezi Minne) bila kufanya kazi, kutokuwa na Ripoti ya utekelezaji wa kazi za Wizara na Ilani ya chama hicho atachukuliwa hatua kwasababu sasa ni wakati wa kuwatumikia Wananchi.

Leave A Reply