The House of Favourite Newspapers

Makontena ya Makonda Yabuma Tena Bandarini

MAKONTENA ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,  leo Jumamosi Septemba 15, 2018 yamekosa tena wanunuzi kwa mara ya nne mfululizo katika mnada uliofanyika bandarini jijini Dar es Salaam.

 

Akizungumza kwenye mnada huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Udalali ya Yono, Scolastica Kevela,  amesema mnada huo umeendeshwa lakini mnunuzi hajapatikana.

 

Aliongeza kwamba hadi sasa bei zinazofikiwa na wateja hazijafikia malengo waliyowekewa  na kwamba wao wakiwa madalali wataendelea kufanya utafiti wa kuwapata wateja.

 

Wateja wachache waliokuwa kwenye mnada huo walionekana kutaja bei lakini hakuna hata mmoja aliyefanikiwa kufikia kiwango kilichowekwa.

Comments are closed.