The House of Favourite Newspapers

Soma Hapa: Makosa Makubwa Wanayoyafanya Wanaume kwa Wanawake Wao Kwenye Mapenzi

0

RAFIKI, je, umewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke halafu mara akapoteza hisia na wewe? Anaonekana siku moja anajisikia na wewe mara ghafla anakwambia amechoshwa na wewe? Unatumia mbinu zako zote za maujanja kumfanya arudishe maslahi kwako, lakini ni kama kupigia mbuzi gita.

 

Mwishowe anakataa kujibu au kupokea simu zako. Au anakutumia ujumbe; “Kuanzia leo naona heri tuwe marafiki tu!”

Je, unadhani tatizo hapa linakujaje? Tatizo ni kuwa utakuwa umelileta wewe mwenyewe. Kujaribu kutopatikana na majanga kama haya tena, nimeamua kuorodhesha makosa makubwa wanaume hufanya kwa mwanamke;

 

Kujaribu kumpendeza; kama unashangaa inawezekanaje kumpendeza mwanamke ikawa kosa kubwa la kumfanyia mwanamke, basi ni dhahiri kuwa wewe umewahi kufanya kosa kama hilo.

 

Kwa hiyo makosa makuu ya kumpendeza mwanamke ni nini? Mara nyingi huletwa na sababu mbili kuu; kuzungumza sana kujihusu -wanaume wengine wakiwa wanaongea na mwanamke kazi yao sana ni kujieleza kuhusu maisha yao, matukio waliyoyafanya n.k bila ya kumpa mwenzake nafasi ya kujieleza.

 

Hebu chukulia unazungumza na mtu ambaye anaongea yeye peke yake bila kukupa nafasi ya kumjibu.

Kujisifu na mali ulionayo –hili ni kosa lingine, kuwa na tabia ya kujisifu kuhusu vitu unavyomiliki. Ingawa wewe utaona ni sifa, kwa mwanamke huwa ni tofauti kabisa.

 

Kukubaliana na kila kitu atakachosema; mwanaume ambaye hana uwezo wa kukataa chochote kutoka kwa mwanamke, basi ni ishara ya kuwa baada ya muda mfupi wa uhusiano wao wa kimapenzi, wataachana.

 

Kwa mujibu wa saikolojia ya wanawake, wao hupenda kuongozwa na wala si kuongoza. Hivyo wakiona kuwa kila kitu atakachosema mwanaume anakubaliana nacho bila kupinga, basi kwa kawaida huona ya kuwa unataka yeye ndiye aendeleze uhusiano wengu. Pia mara nyingi huona kama kuwa na wewe kimapenzi kunaboa.

 

Hapa nataka ufahamu ya kwamba sijasema lazima upinge kila kitu mwanamke anachosema wala sijasema uanze vita na mwanamke ili kukabiana na changamoto ya kutemwa. La hasha! Mwanamke kawaida anapenda vioja katika maisha yake.

 

Leo ukiwa na tabia hii, kesho mgeuzie tabia nyingine. Huku kutayafanya maisha yenu yawe ya kuvutia kila wakati.

 

Kuitikia mahitaji yake kila wakati; je, wewe ni yule mwanaume ambaye akipigiwa simu na mpenzi wake anaacha shughuli zake zote ili kumjibu? Ama wewe ni aina ya mwanaume ambaye kila mahali mpenzi wako atakapokwenda unakuwa kando yake?

 

Labda unaona kufanya hivi unatimiza tabia za kuwa kama gentleman au unajaribu kumridhisha mpenzi wako. Ikiwa hizi ni baadhi ya tabia unazofanya basi elewa ya kuwa hauko mbali kuachwa na mpenzi wako.

 

Hii ni kwa sababu itafikia mahali f’lani mwanamke atakushusha hadhi kwa kuwa atakuona huna maisha. Ataona kwamba maisha yako yamezungukwa kwake.

 

Ni muhimu kwa mwanaume kuishi maisha yake yeye mwenyewe na wala si kuzungukwa na mwanamke. Hebu chukulia hivi, umemzoesha mwanamke kuwa kila mahali atakuwa akitembea na wewe, je, ikifikia wakati wa kuchukua mkondo wa kuishi maisha yako kivyako itakuwaje?

 

Kumgharamikia anachotaka kupindukia; kuna wanaume wengine wanafanya kosa la kujionesha kuwa maisha yao ni ya juu kwa kumgharamikia mwanamke mahitaji yake yote anayotaka.

 

Hii nikuanzia kumfanyia shopping, kumtoa auti na kumpeleka sehemu za gharama nk.

Labda ni kweli kipesa huna tatizo, lakini fahamu ya kuwa itafikia mahali f’lani mwanamke ataanza kukushuku kama kweli wewe mapenzi yako ni ya dhati au upo tu kumtumia, halafu baada ya hapo unaachana naye.

 

Halafu pia ukimzoesha mwanamke kuwa kila wakati utakuwa ukimtolea pesa ikitokea kwa bahati mbaya ukose pesa, basi uhusiano wenu wa kimapenzi utakuwa na shida.

 

Unamgojea yeye aanze kuonesha maslahi kwako; huyu mwanamke unampenda, lakini hutaki kumwambia kuwa umemzimia. Unamsoma akili na miondoko yake na umegundua kwamba pia yeye amekuzimia. Kwa hivyo unangojea nini?

 

Kosa ambalo wanaume wengine hufanya ni kuwa hawafunguki kwa mwanamke mpaka aone mwanamke anafunguka wa kwanza.

 

Mwanaume kama huyu anacheza karata zake kwa kuangalia hatua gani mwanamke atachukua kama approach.

Kungojea mwanamke aoneshe nia kwako ni kosa kubwa kwani mwanaume ndiye ana majukumu ya kuhakikisha ya kuwa anamtongoza mwanamke na wala si mwanamke kumtongoza yeye.

 

Kwa leo ninaishia hapa, tukutane IJUMAA ijayo kwa mada nyingine tamu.

Mwandishi Maalum; Maoni +255 713 750 910

HAPA KAJALA KAPATIKANA, HARMONIZE AMNUNULIA RANGE ROVER MBILI, AMWAMBIA – “NATAKA MAEX WAKUITE BOSS”

Leave A Reply