The House of Favourite Newspapers

Makosa wafanyayo wapenzi wawapo chumbani-3

0

feng-shui-love-tips-resized-6001Ni matumaini yangu kwamba msomaji wangu u mzima wa afya. Ni Ijumaa nyingine ninapokukaribisha katika ukurasa wetu huu mzuri. Tunaendelea na mada yetu tuliyoianza wiki mbili zilizopita, inayohusu makosa wayafanyayo wanandoa/wapenzi wawapo chumbani. Tuliishia kuelezea kipengele cha tano kinachohusu usafi. Endelea…

Utashangaa baadhi ya wanawake wanapendeza wanapoenda kuwatembelea ndugu, jamaa, marafiki au wanapoenda kwenye shughuli lakini wanakuwa wachafu wanapopanda vitandani na wenzi wao. Usafi ni kitu muhimu.

Kwa wanaume pia, wapo wenye kawaida ya kunywa pombe na kurudi wakiwa wanatoa harufu kali, badala ya kupata japo muda kidogo wa kuoga vizuri na kupunguza harufu ya pombe, wanapanda vitandani wakiwa wananuka pombe utafikiri wanafanya kazi viwanda vya pombe. Kama na wewe ni miongoni mwa watu wa aina hii, hujachelewa! Badilika kwa sababu inawezekana.

6. KUWA NA VISINGIZO VINGI KUHUSU TENDO
Upo ushahidi wa wanandoa ambao wana kawaida ya kukwepa kuwapa wenzi wao haki ya ndoa wanapohitaji. Yaani muda wa kulala ukifika, yupo radhi hata achukue nguo akaanze kufua ili akirudi akute mwenzi wake ameshalala. Mwingine anajifanya yupo bize na kazi za ofisini ilimradi tu hataki kuguswa na mwenzi wake.

Hakuna kosa kubwa linalosababisha ndoa nyingi kuvunjika kama wanandoa kushindwa kutimiziana haja zao za msingi hususan katika tendo la ndoa.

Kama kuna jambo limesababisha ukakosa hamu ya kukutana na mwenzio ni bora mkajadiliana kwa upole na kutafuta namna ya kulishughulikia kwa sababu wakati mwingine, baadhi ya wanandoa hukosa hamu ya tendo (hasa wanawake) kutokana na matatizo ya kisaikolojia au kimaumbile.

Kama hutaki kukutana naye kwa sababu unajua atakuacha njiani kama alivyofanya juzi na jana, kumkwepa siyo suluhisho bali mnaweza kukaa na kulizungumzia tatizo lililosababisha ukawa na hali hiyo. Yapo malalamiko ya baadhi ya wanaume kwamba wake zao hawaishi visingizio linapokuja suala la kuwa faragha, asiposema anaumwa kichwa basi atasema anaumwa tumbo au amechoka.

Matokeo yake mnasababisha ufa na baadaye mmoja anaona ni bora atafute mchepuko wa kumtuliza kuliko mateso anayoyapata ndani kwa kulazwa na njaa kila siku.

7. KWENDA KULALA UKIWA NA HASIRA
Hakuna kitu kibaya kama kupanda kitandani huku ukiwa na hasira, iwe aliyezisababisha ni mwenzi wako au ni mtu mwingine yeyote. Wapo baadhi ya watu ambao kwa sababu siku hiyo alifokewa na bosi wake kazini, basi kutwa nzima anashinda akiwa na hasira na hata muda wa kulala ukifika, anapanda kitandani akiwa na kisirani.

Wachambuzi wa masuala ya mapenzi, wanaeleza kuwa hii ni sumu mbaya ambayo kama unaipenda ndoa yako ni lazima upambane kuhakikisha unaachana nayo. Kuna usemi maarufu usemao, yaache matatizo ya kazini kwako kazini na yaache matatizo ya nyumbani kwako nyumbani.

Hata kama siku yako ilikuwa mbaya ni makosa kwenda kummalizia hasira mwenzi wako. Pia kama mwenzi wako ndiye aliyesababisha uwe na hasira, usikimbilie kwenda kulala na hasira zako ukidhani kwamba hilo ndiyo suluhisho. Hata kama umekasirika kiasi gani, jipe muda wa kutulia kisha zungumza na mwenzi wako kuhusu kilichosababisha ukakasirika.
Kwa maoni na ushauri nicheki kwa namba zilizopo hapo juu.

Leave A Reply