The House of Favourite Newspapers

Malaika: Sifikirii kabisa kuolewa

0

MALAIKAStori: BONIPHACE NGUMIJE

MSANII wa Bongo Fleva, Diana Exavery ‘Malaika’ amesema kuwa  kwa sasa miongoni mwa mambo ambayo hayafikiria kabisa ni kitu kinachoitwa mapenzi haswa ndoa na badala yake ameweka akili yake yote kwenye kazi yake ya muziki ili atoboe zaidi pamoja na masuala ya ujasiriamali.

Akipiga stori mbili tatu na Risasi Jumamosi, Malaika alisema kuwa jambo ambalo ameligundua ni kwamba si busara kuchanganya mambo mengi kwa wakati mmoja na kuongeza kuwa umri wake bado ni mdogo kukimbilia kwenye ndoa na anatakiwa kuandaa mustakabali wa maisha yake ya baadaye kwa sasa.

“Sifikirii kabisa kuhusu ndoa, yaani hata mshipa haunigongi, nawaza kazi tu na jambo lingine ambalo napenda kuliweka wazi ni hata kuwa kwenye uhusiano tu sihitaji. Hapa kazi tu ndiyo suala ambalo nimeliweka mbele kwa sasa,” alisema Malaika.

 

Leave A Reply