The House of Favourite Newspapers

Uwoya: Mtoto wa pili nazaa na Ndikumana

0

Irene_Uwoya028Stori: IMELDA MTEMA, Risasi Jumamosi

DAR ES SALAAM: Staa mwenye mvuto wa kipekee Bongo Muvi, Irene Uwoya amefanya mahojiano ‘exclusive’ na gazeti hili ambapo moja ya jambo la kushangaza aliloliongea ni kwamba, akitaka kuzaa mtoto wa pili atamtafuta mumewe, Hamad Ndikumana azae naye.

Uwoya na Ndikumana ambaye ni raia wa Rwanda walifunga ndoa mwaka 2009 na kujaaliwa kupata mtoto mmoja aitwaye Krish kisha wakazinguana na kutengana mwaka 2013.

UWOYANANDIKUNACRISHIII Unataka kujua aliulizwa nini, akajibu vipi? Fuatilia mahojiano hapa chini…

Risasi: Tangu ndoa yenu iparaganyike unaonekana ukiwa peke yako, hivi Ndikumana siku hizi yuko wapi?

Uwoya: Mh! Kwa kweli mimi sijui yuko wapi.

Risasi: Unashindwaje kujua yuko wapi wakati tayari ni mzazi mwenzako?

Uwoya: Sijui tu, inawezekana yuko kwao.

IRENE 23Risasi: Kwa hiyo ndoa yenu ndiyo basi tena?

Uwoya: Tangu lini ndoa ya Kikristo ikavunjika, tupo ila kila mtu yuko kivyake.

Risasi: Sasa katika mazingira hayo huoni kwamba siyo sahihi?

Uwoya: Hapana, mimi naona sawa tu.

Risasi: Kwa hiyo una mtu mwingine?

Uwoya: Ndiyo na yeye atakuwa na mtu mwingine.

Risasi:  Sasa katika hilo wazazi wa Ndikumana wanasemaje?

Uwoya: Hawapendi hata kunisikia lakini kwa vile Hamad bado ananipenda, hawanisumbui.

Risasi: Vipi sasa ukitaka kuongeza mtoto mwingine?

Uwoya: Nikitaka kuongeza mtoto wa pili nitamtafuta Hamad maana sipendi kuchanganya baba kwa watoto wangu.

Leave A Reply