The House of Favourite Newspapers

Mama Amlilia JPM: ‘Mwanangu Amelawitiwa’, Rais Ampa Mil 1, Aagiza Haya – Video

RAIS John Magufuli amempa msaada wa kiasi cha Tsh milioni 1, mama mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Swaumu ambaye amemlilia Rais akidai mtoto wake amelawitiwa na yupo katika hali mbaya ya kiafaya na hapati msaada kutoka kwenye vyombo vya usalama.

 

Magufuli amefanya uamuzi huo Aprili 26, 2019, jijini Mbeya wakati wa mkutano wake wa hadhara na wananchi wa mkoa huo waliojitokeza katika katika viwanja vya Ruanda, Nzovwe,  baada ya mama huyo kujitokeza na kuanza kulalamika mwanaye kufanyiwa tukio hilo la kinyama.

 

“Mheshimiwa rais, nina mwanangu amelawitiwa na mtu ana miaka 53, kesi ilipoanza polisi wakasema mtoto ni mwanamme na ana umri wa miaka 20, mwanangu ni wa kiume na picha nimekuja nazo hapa, nimeshindwa kufika naye kwa sababu anajiharishia kutokana na hali aliyonayo, ameumizwa sana… Sina msaada, nimechaniwa mabango tangu jana na leo wakitaka nisikueleze kero hii mheshimiwa,” alisema mama huyo.

 

Baada ya kumsikiliza, rais  alimpa Tsh milioni moja na kuliagiza jeshi la polisi kuanza upya uchunguzi wa kesi hiyo huku akimtaka mama huyo kumkabidhi nyaraka na picha msaidizi wa rais wa masuala ya sheria ili alifanyie kazi haraka.

 

VIDO: FUATILIA TUKIO HAPA

Comments are closed.