The House of Favourite Newspapers

Mama Atoa Neno Wema, Aunt Kutifuana

0

BAADA ya hivi karibuni mastaa wa filamu waliokuwa mashosti, Wema Sepetu na Aunt Ezekiel kugombana, na sasa hakuna anayezungumza na mwenzake, mama Wema, Miriam Sepetu ameibuka na kutoa neno.

 

Akipiga stori na Amani, mama Wema alisema katika urafiki wa mwanaye na Aunt, walikuwa wakigombana mara kwa mara na kupatana, kwa hiyo hashangai hivi sasa ambavyo wamegombana.

 

Aidha alisema hawezi kumchagulia rafiki Wema kwa kuwa ni mtu mzima mwenye kujua mema na mabaya, akiona anayemfaa kuwa na urafiki naye basi anaweza kuwa naye.

 

“Kwenye urafiki wa Wema na Aunt walikuwa wanagombana na kupatana kila wakati, hivyo hata sasa siwezi kushangaa na wala sijashangaa kutoelewana kwao pia siwezi kumpangia awe na rafiki huyu ama yule,’’ alisema mama Wema.

 

Licha ya kuapa kwamba urafiki wao utatenganishwa na kifo, hivi karibuni Wema na Aunt waliingia kwenye bifu, huku chanzo kikitajwa kuwa ni ugomvi uliousababisha ndugu mmojawapo wa Wema.

 

Baada ya urafiki huo kufa, Wema amekuwa akionekana akiwa karibu na msanii wa muziki wa kizazi kipya, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’.

Stori: Happyness Masunga

Leave A Reply