The House of Favourite Newspapers

Tanasha Kumburuza Diamond Mahakamani, Ataka Mali Nusu kwa Nusu

0

MREMBO na mwanamuziki, raia wa Kenya, Tanasha Donna, anasemekana amempeleka mwanamuziki nyota wa Tanzania, Diamond Platnumz, mahakamani akitaka wagawane mali alizonazo nusu kwa nusu kwa kuishi naye kama mke na mume.

 

Kwa mujibu wa mtandao wa Galaxy FM.Co.UG wa nchini Uganda, Tanasha, aliyekuwa mpenzi wa Diamond kwa miaka miwili, na wakajaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume, lakini wakaachana hivi karibuni, amedai mwanamme huyo ana tabia ya kuzaa watoto na wanawake ambao huwatelekeza.

 

Hivi sasa mahakama husika nchini Tanzania (bado haijatajwa) inadaiwa kuelekeza  kwamba mgawanyo wa mali hiyo utategemea mchango wa mrembo huyo moja kwa moja au kwa njia nyingine katika mali husika.  Pia inasemekana kueleza kwamba upande wa madai lazima uthibitishe mchango huo katika mali hizo.

 

Inasemekana jaji mwenye kuhusika na suala hilo alitoa maelekezo hayo katika msingi huo ambao huamua mashtaka ya watu waliokuwa wanandoa wanapogombea mali baada ya kuachana.

 

Katika makabiliano hayo Tanasha amepewa nusu ya haki ya makazi na mali zinazotokana na  watu wawili kuishi kama mume na mke lakini si mgao wa mali anazomiliki Diamond, jambo ambalo lilimfanya Tanasha akimbilie mahakamani.

 

Katika mlolongo huo, Diamond aliorodhesha mali za aina tatu — viwanja viwili jijini Dar es Salaam, kituo cha radio na kituo cha televisheni ambapo Tanasha aliapa mahakamani kwamba alikuwa na mchango wa kifedha na usio wa kifedha katika manunuzi au mwendelezo wa mali zote hizo.

 

Alisisitiza zaidi kwamba alitoa fedha katika ujenzi wa makazi na mali walizotumia wakiishi pamoja. Akitoa ushahidi, mwanamke huyo mwenye haiba ya kuvutia, alisema mchango wake aliutoa kupitia vitegauchumi vya kibiashara vilivyokwenda katika upanuzi  wa Kituo cha Radio cha  Wasafi.

Leave A Reply