The House of Favourite Newspapers

Mama Diamond kurudi Tandale, kumpisha Zari

3

zariii Zarinah Hassan ‘Zari’ au mama Tiffah.

KUNA madai kwamba, mama wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kasim ‘Sandra’ yupo katika maandalizi ya kuhamia kwenye makazi ya Tandale alikokuwa akiishi zamani ili kumpisha mwanye na mama mtoto wake, Zarinah Hassan ‘Zari’ au mama Tiffah kwenye makazi ya Madale jijini Dar.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, mama huyo au bibi Tiffah amefikia uamuzi huo ili kuepusha lolote linaloweza kutokea kwa kukaa beneti na mkaza mwanaye kwa vile ulimi hauna mfupa wala macho hayana pazia.

“Jamani mnajua kama mama Diamond anataka kurudi kuishi Tandale alikotoka. Anampisha Zari na Diamond wake watanue kwenye mjengo wa Madale. Si unajua wamemzaa Lattifah ‘Tiffah’, ndiyo maana yule mama hivi karibuni kwenye moja ya magazeti yenu (Risasi Jumamosi) mlitoa habari na picha akisimamia ukarabati wa ile nyumba ya Tandale,” kilisema chanzo.

mama-diamondKikaendelea: “Asichotaka yule mama ni kuzozana na mkaza mwanaye. Unajua yeye ni mtu mzima, sasa kupishanapishana Kiswahili na binti kama Zari si sawasawa.”
Amani lilimtafuta msemaji wa familia hiyo ambaye ni Diamond mwenyewe na kuulizwa kuhusu madai hayo, alisema:

“Hamna kaka. Ile nyumba ni ya familia. Nimeamua kuikarabati kwa sababu ni ya familia. Mimi nina mama, nina dada zangu, isingekuwa rahisi nianze kuikarabati nyumba ya Tandale ambayo ni ya wote. Ndiyo maana nilianza kujenga yangu kwanza kisha ya familia. Hata mama akienda kuishi kule kwani tatizo liko wapi? Si nyumba yetu?” alisema Diamond.

3 Comments
  1. breckii says

    hivi huyu zari ni binti au ni bibi, mwandishi tufafanulie

    1. winnie s says

      Jmn unae uriza Zari in Bibi.uko sawa kichwani.Zari akiwa Bibi.Na Mama D atakuwa nani.acha zarau za hivo.mwandishi usifafanue chochote.

      1. Alex kihongole says

        Kipenda roho

Leave A Reply