The House of Favourite Newspapers

Bomoa bomoa mahekalu Dar, ripoti inatisha

0

1Tingatinga likiendelea na kazi ya ubomoaji.

HALI tete! Kufuatia Mahakama ya Ardhi, Dar kutengua bomoabomoa ya nyumba 674, bado ripoti inatisha kwa zile nyumba ambazo mahakama haikuzitambua na zile ambazo zilishabomolewa mwishoni mwa mwaka jana.

1222

Moja ya mjengo wa ukibomolewa.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa wengi waliokimbilia mahakamani, walikuwa wakisukumwa na baadhi ya vigogo wenye mahekalu yao maeneo ya Mbezi, Dar ambao walikuwa wanashindwa kujitokeza mstari wa mbele kwa kuhofia kuhojiwa au kujulikana nyumba zao ambazo walikuwa wakizimiliki kwa siri.

Imebainika kuwa baadhi ya vigogo hao ni wale wanaofanya kazi serikalini ambapo mijengo yao haifanani na mishahara wanayoipata hivyo kuingia kwenye ‘figisufigisu’ ya uhujumu uchumi.

Ardhi - 6

…….Tingatinga likifanya yake.

Wakati hali ikiwa hivyo, imebainika kuwa mfanyabiashara maarufu jijini Dar, Muzamil Katunzi ni miongoni mwa watu ambao wamekumbwa na sekeseke hilo baada ya kubomolewa uzio wa kiwanja chake kilichopo Mbezi Beach.

Naye bosi wa Kampuni ya Udalali ya Majembe Auction Mart aliyejulikana kwa jina moja la Mwamoto, anayemiliki nyumba eneo la Mbezi, yeye ameamua kubomoa mwenyewe sehemu ya ukuta wa nyumba yake kabla ya serikali kuingilia kati ili aweze kunusuru mali zake.

BOMOABOMOA-2Hata hivyo, katika hali isiyokuwa ya kawaida, mahekalu mengi ya watu wanaodaiwa kuwa ni baadhi ya vigogo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), hayajawekewa alama ya X ‘bomoa’ kufuatia kujengwa umbali wa mita 60 kutoka baharini ambapo ndiyo sheria inavyotaka.

Juzi, kwenye Mahakama ya Ardhi, korti ilisema inatambua nyumba 674 tu zilizopo Wilaya ya Kinondoni, Dar ambazo zina pingamizi la kisheria.

DSC_1051Kwa mujibu wa mahakama, kesi kuhusu pingamizi la nyumba hizo itatajwa mahakamani Jumatatu, Januari 11, 2016. Nyumba hizo 674, mahakama imesema hazitakiwi kuguswa na bomoabomoa kwa sababu upande wa serikali haujatoa vibali vinavyotosheleza kuifanya mahakama iamuru zibomolewe.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, nyumba ambazo mahakama haikuzitambua, serikali itaamua yenyewe inabomoa lini kulingana na utaratibu wake.

“Sasa hivi tunabomoa maeneo ya Mbuyuni na Hananasif, maeneo mengine kama Mbezi Beach na kwingineko, tunasubiri maelekezo kutoka ngazi za juu,” Arnold Kisiraga, Afisa Utunzaji wa Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Uhifadhi wa Mazingira (NEMC) aliliambia Amani.

mbeziKatika uchunguzi wa gazeti hili, imebainika kwamba baadhi ya vigogo ambao nyumba zao zipo kwenye mkumbo wa kubomolewa, wameshaanza kutafuta makazi Uswahilini, wengine wanahamisha vyombo vyao wakikwepa kupata hasara.

“Wengi wanalia, wengine wamepata presha kwa vile baada ya bomoabomoa hawajui watakwenda wapi,” kilisema chanzo chetu.

Waandishi: Issa Mnally, Boniphace Ngumije, Chande Abdallah na Makongoro Oging’.

Leave A Reply