The House of Favourite Newspapers

MAMA KANUMBA: SETH ALIVISHINDWA VIATU VYA KANUMBA

Bi. Frola Mtegoa

MAMA mzazi wa aliyekuwa msanii wa filamu za Bongo, marehemu Steven Kanumba, Bi. Frola Mtegoa ‘mama Kanumba’ amesema baada ya kifo cha mwanaye huyo alidhani huenda mtoto wake mwingine, Seth Bosco angeweza kuvaa viatu vya kaka yake lakini amevishindwa.

Akipiga stori na Star Showbiz, mama Kanumba alisema kuwa;“Baada ya kifo cha mwanangu Kanumba ukweli kila kitu kilivurugika si unajua muanzilishi ni muanzilishi tu nikajua mimi na mwanangu Seth tungeweza kuindeleza lakini baadaye tulishindwa maana Seth alishindwa kuvaa viatu vya marehemu kaka yake kama nilivyotegemea.

“Lakini naomba niwaambie kwamba tuko kwenye michakato ya kuifufua kampuni hiyo baada ya kuzisoma chalenji nyingi za tasnia hii ambapo awali sikuwa na uzoefu kama nilionao sasa,” alisema mama Kanumba.

 

RICHARD BUKOS

Comments are closed.