The House of Favourite Newspapers

Mama Mjane Asimulia Mumewe Kulawiti Mabinti Zake Wawili, Atupwa Jela Miaka 60 – Video

0

Maisha yana siri nzito nyuma ya pazia Global TV inakuletea kisa kizito cha mwanamke ambaye mabinti zake wawili wamelawitiwa na baba yao wa kufikia huku mmoja akipewa ujauzito.

Akisimulia kwa uchungu mkasa huo, mwanamke huyo ameeleza kuwa baada ya suala hilo kufikishwa kwenye vyombo vya sheria na ushahidi wa vinasaba (DNA) kuthibitisha kwamba mumewe ndiye aliyempa ujauzito binti yake wa kwanza na kumwingilia binti yake mwingine mara kwa mara, mwanaume huyo alihukumiwa kifungo cha miaka 60 jela.

Hukumu hiyo ikazalisha tatizo lingine kwani mwanamke huyo anaeleza kwamba amebaki na mzigo wa kuwalea wanaye watano na wajukuu wawili, akiwa hana kazi wala kipato cha kumuwezesha kumudu malezi hayo.

Kodi ya nyumba anayoishi na wanaye imeisha na hata chakula kwa wanaye imekuwa mtihani mzito kwake kiasi cha kuwaomba Watanzania wamsaidie kwa hali na mali.

Leave A Reply