The House of Favourite Newspapers

Jenerali Mabeyo Afunguka A To Z Kifo Cha Rais Magufuli – Video

0
Aliyekuwa Mkuu wa Majeshi nchini Jenerali Mstaafu Venance Mabeyo.

LEO Machi 17, mwaka huu Tanzania tunaidhimisha miaka mitatu tangu kifo cha Rais John Magufuli. Rais wa Kwanza kufariki Dunia akiwa madarakani katika historia ya Tanzania.

Aliyekuwa Mkuu wa Majeshi nchini Jenerali Mstaafu Venance Mabeyo ambaye amefunguka saa 24 za kabla ya Magufuli kuaga Dunia na saa 40 kabla ya Rais Samia Suluhu Hassan kuapishwa kuwa Rais wa awamu ya Sita katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali Venance Mabeyo amesema siku moja kabla ya kifo cha Hayati John J. Magufuli, alimwita na kumwambia anajua hawezi kupona na hivyo awaagize Madaktari wamrudishe nyumbani kwake

Mabeyo amesema “Aliniita CDF njoo, siwezi kupona, waamuru hawa Madaktari wanirudishe nyumbani. Nikamjibu Mheshimiwa sina Mamlaka hayo, suala la Afya sio la CDF, naomba ubaki Madaktari watatuambia”

Ameongeza kuwa Machi 17, 2021 saa 8 mchana, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama waliambiwa hali ya Rais Magufuli imebadilika na ilipofika saa 12:30 Jioni alifariki

Leave A Reply