The House of Favourite Newspapers

Mama Mlezi wa Rais Jakaya Kikwete Azikwa Bagamoyo

Mwili wa Marehemu, Bi. Nuru Khalfan Kikwete ukiwasili nyumbani kwake, mtaa wa Top Life Bagamoyo baada ya kutolewa hospitali ulikokuwa umehifadhiwa.

Rais Kikwete akizungumza na baadhi ya wanafamilia na waombolezaji nyumbani kwa marehemu.

Kikwete akijadiliana jambo na baadhi ya ndugu na waombolezaji.

Mke wa Rais Kikwete, Mama Salma Kikwete akishauliana jambo na mmoja wa wanafamilia.

Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubakar Zuberi Bin Ally akizungumza jambo wakati wa maombolezo hayo.

Rais Kikwete akisalimiana na mmoja wa waombolezaji.

Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akijumuika na waombolezaji wengine msibani hapo.

Jaji Mkuu, Othman Chande akiteta jambo.

Steven Wassira akiwa msibani.

Meya wa Jiji la Dar, Isaya Mwita Charles (mwenye koti jeusi) akijumuika na waombolezaji wengine

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na waombolezaji.

Mwili wa marehemu ukiswaliwa kabla ya kuzikwa katika makaburi ya Mwakarenga, Bagamoyo.

MAMA Mlezi wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Bi. Nuru Khalfan Kikwete, aliyefariki  asubuhi jana asubuhi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa matibabu, amezikwa leo katika makaburi ya Mwanakarenga, Bagamoyo, Pwani.

PICHA ZOTE NA HILLARY DAUDI | GOBAL PUBLISHERS

Comments are closed.