The House of Favourite Newspapers

Samia Atoa Maagizo Serikali za Mitaa – Video

0

 

MAKAMU  wa Rais, Samia Suluhu, ametoa wito kwa serikali za mitaa kuhakikisha kamati zake za maji zinalinda miundombinu ya maji pamoja ili Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) iweze kuboresha huduma zake.

 

Ametoa wito huo leo jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kutembelea Mradi wa Maji wa Pugu- Gongo la Mboto, tukio lililofanyika katika Shule ya Sekondari ya Pugu na kuzitaka kamati hizo kusimamia kikamilifu watumiaji wa huduma hiyo kulipa bili kwa wakati.

 

 

“DAWASA kwa sasa tumewapeleka hadi Mkoa wa Pwani hatukutaka kuwafunga katika mkoa wao, pia wameenda hadi Same na Mwanga na wamepewa jukumu hilo kutokana na utendaji wanaofanya, hivyo miundombinu ikitunzwa na wateja wakilipa bili zao kwa wakati huduma zao zitaboreka,” alisema Suluhu.

 

 

Aidha, amewataka wananchi kuwapuuza wachuuzi wa maji ambao hawafurahii upatikanaji wa maji kwa kuharibu na kufanya mbinu nyingi ya kuwarubuni wananchi kuwa bili za DAWASA ni kubwa huku wakihusika na uhujumu wa miundombinu.

 

Leave A Reply