The House of Favourite Newspapers

Mama Samia Awasili Serengeti Kuadhimisha Miaka 60 ya TANAPA

0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adama Malima alipokuwa Uwanja wa Ndege wa Seronera Wilaya ya Serengeti leo Desemba 22, 2019 kwa ajili ya kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 60 ya kuanzishwa kwa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) yanayotarajiwa kufanyika kesho katika Hifadhi ya Ikoma, Serengeti mkoani Mara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangala.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amepokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Seronera Wilaya ya Serengeti leo Disemba 22, 2019 kwa ajili ya kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 60 ya kuanzishwa kwa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na Mamlaka ya Hifadhi ya NGORONGORO (NCAA) yanayotarajiwa kufanyika kesho katika Hifadhi ya Ikoma Serengeti mkoani Mara.

Leave A Reply