The House of Favourite Newspapers

MAMBO 5 YA AJABU BINADAMU ANAWEZA KUYAFANYA (PICHA)

Kwa baadhi ya imani za walio wengi wanaamini kwamba kila binadamu yupo sawa lakini kuna wengine wanapinga jambo hilo.

 

Kiukweli sio binadamu wote tupo sawa kwa sababu kuna mambo ambayo yanafanywa baadhi ya watu flani na kwa upande wako hauwezi kulifanya jambo hilo hata ukijaribu kwa muda mrefu.

 

Leo utayajua mambo matano ya kushangaza ambayo kwa mujibu wa takwimu, ni asilimia 3 tu ya binadamu wote duniani wanaweza kuyafanya.

 

5: Ulimi Kugusa Pua

Asilimia chahe sana ya watu duniani wanaweza kufanya jambo kama hili (jaribu)

 

  • #JIFUNZE

Unachotakiwa kufanya ni kutoa ulimi wako kuuelekezea juu kwenye pua, halafu chukua vidole vya mkono wako usaidie ulimi  kuupandisha. Ukijaribu kila siku utaweza kufanya hvyo.

 

4KUNYANYUA NYUSI MOJA

Ni rahisi sana kunyanyua nyusi mbili kwa wakati mmoja, na asilimia kubwa sana ya binadamu wanaweza kufanya hivyo lakini tunapojaribu kunyanyua kope moja huku nyingine ikiwa pale pale bila kuyumba ni asilimia chache  sana ya binadamu wanaweza kufanya hilo (JARIBU).

 

  • #JIFUNZE

Hakikisha unashika nyusi ya jicho moja kuelekea juu na nyingine kuielekeza chini pale ilipokuwepo kwa kutumia mkono mwingine. Jaribu kufanyia mazoezi kwenye kioo na utajua ni msuli gani unaotakiwa kufanya hivyo.

 

3: KULAMBA KIWIKO CHA MKONO

Kwa baadhi ya binadamu walio wengi wanaweza kufanya hivi lakini wapo wale ambao kufanya jambo hili kunawapa shida sana huku wakiona kwamba ni jambo ambalo haliwezekani kabisa. (JARIBU)

 

  • #JIFUNZE

Fanya mazoezi kwa kujaribu kulamba kiwiko cha mkono wako kila pande huku ukijaribu kama picha ya kwanza juu inavyokuelekeza na mwisho utaweza kufanya hivyo.

 

2: KUTINGISHA MASIKIO

Jambo hili limegundulika asilimia ndogo sana ya binadamu wanaweza kulifanya lakini ni jambo rahisi sana kwa kila mwanadamu kuweza kulifanya endapo atajaribu na kujua misuli inayohusika(JARIBU)

 

  • #JIFUNZE

Isikilize misuli ambayo inahusika na masikio kama ulivyofanya namba 1 kwenye nyusi halafu tabasamu kama picha inavyoonyesha na utaona masikio yanasogea/kucheza. Au unaweza kuchezesha meno ya chini na juu kwa kupeleka upande wa kushoto na kulia,utahisi maskio yanacheza.

 

1: KUPASUA YAI

Kauli hii itakushangaza sana lakini sio kama unavyofikiri kwasababu kuvunja yai kwa wimbo ni jambo ambalo asilimia kubwa sana ya watu hawawezi kufanya hivyo hata kama wakifanya mazoezi zaidi ya miaka 10. (JARIBU)

  • #JIFUNZE

Jaribu kushika yai kama picha inavyokuelekeza na hakikisha vidole vingine vipo chini huku unasogeza vidole viwili taratibu na mwishowe yai litavunjika kwa wima.

 

Nadhani umefurahia baadhi ya Trick/mambo ambayo yalikuwa hayawezekani kwako lakini umejitahidi na umeweza kuyafanya japo sio yote lakini ukiwafanyia rafiki zako wanaokuzunguka lazima watakushangaa na watataka kujua au watakuona mtu wa tofauti.

AKILIMALI “AMUNIKE Angepitia Moja kwa Moja Nigeria Asingerudi”

Comments are closed.