ODEMBA KUMZALIA DIAMOND MTOTO WA 4!

 HISIA! Mwanamitindo anayeipeperusha vyema Bendera ya Tanzania duniani, Miriam Odemba, ametoa lililoko moyoni mwake kwa kusema, yupo tayari kumuongezea Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ mtoto wa nne endapo msanii huyo ataridhia, Ijumaa Wikienda lina ‘full’ stori.  

 

Miriam aliitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita alipokuwa akifanya mahojiano maalum ya moja kwa moja na Ijumaa Wikienda kwa njia ya simu kutokea nchini Ufaransa ambako anaishi mwanamitindo huyo.

 

Katika mahojiano hayo yaliyohusu mambo mbalimbali, Miriam alijikuta akimfungukia Diamond kwa kusema amekuwa akiangalia mwenendo wake na kumuona ni ‘baba bora’ hivyo si vibaya akimzalia mtoto mmoja.

 

Image result for MIRIAM ODEMBA NA DIAMOND PLATNUMZ

Kwenye mahojiano hayo, Odemba alisema anafuatilia watoto wa Diamond, wale wawili aliozaa na mwanamama mjasiriamali wa Kiganda, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ na yule wa mwanamitindo Hamisa Mobeto na kugundua anawalea vizuri, kitu ambacho kinamshawishi na yeye awe tayari ‘kumtunuku’.

 

TUPATE MAHOJIANO KAMILI

Ijumaa Wikienda: Vipi Miriam, habari za huko?

Odemba: Salama kabisa, vipo Bongo mambo yanakwendaje?

Ijumaa Wikienda: Huku shwari, vipi una mpango wa kurejea nyumbani au ndiyo huko maisha yako moja kwa moja?

Odemba: Nitarudi lazima maana Tanzania ni nyumbani, nakupenda mno huko, huku ni maisha tu.

Ijumaa Wikienda: Kitu gani cha nyumbani ambacho unavutiwa nacho ukiwa huko?

Odemba: Kwa kweli mimi napenda sana muziki hicho ndicho kitu kikubwa kinachonifanya nikumbuke nyumbani, hata hivi nipo huku huwa najisikia raha sana nikisikiliza nyimbo za Diamond, napenda mno mpaka nachanganyikiwa.

 

Ijumaa Wikienda: Kwa nini unapenda za Diamond na wengine vipi?

Odemba: Hapana, siyo kwamba nyingine sipendi, lakini Diamond nampendaga pia anavyojua kuangalia watoto wake mpaka kuna wakati natamani mimi ningezaa naye mtoto mmoja.

Ijumaa Wikienda: Kwa nini upo tayari kumzalia Diamond na si msanii mwingine yeyote?

 

Odemba: Ni kijana mdogo, lakini anaweza kujali familia yake na watoto wake japokuwa hayupo vizuri na mama wa watoto hao (Zari na Mobeto), hapo ndipo anaponikosha sana.

Ijumaa Wikienda: Ni kitu gani hasa anachokuwa anakifanya kwa watoto wake kinakuvutia?

Odemba: Unajua mara nyingi naweza kumuona anatoka Tanzania na kwenda Sauz (Afrika Kusini), kwa ajili ya kuona watoto wake japokuwa hayuko tena kwenye mapenzi na mzazi mwenzake.

WALIVYOKUTANA…

Ijumaa Wikienda: Ulishawahi kuonana uso kwa uso na Diamond?

Odemba: Ndiyo, nilikutana naye alipokuja Ufaransa, tukawa naye, nilifurahi sana na tulikutanishwa na Salam SK (mmoja wa mameneja wa Diamond) kwa hiyo mpaka leo ni mtu ambaye namuelewa sana.

Ijumaa Wikienda: Vipi ushawahi kutamani labda ungezaa naye wewe kabla hajakutana na hawa akina Mobeto na Zari?

 

Odemba: Unajua hakuna mwanamke asiyependa baba kama Diamond na mimi nimezungumzia kwa kuona ni kijana anayejituma sana na hiyo ni kwa ajili ya watoto wake.

Ijumaa Wikienda: Tunafahamu huko ulikuwa unaishi na baba watoto wako Mzungu ambaye mlimwagana, vipi mmesharudiana?

Odemba: Hapana, lakini najua Mungu atafanya wepesi.

 

Ijumaa Wikienda: Tunafahamu kuhusu kampeni yako ya Run With Odemba iliishia wapi?

Odemba: Hicho kitu ninatarajia kuja nyumbani hivi karibuni nitaiendeleza.

Ijumaa Wikienda: Sawa, asante sana.

 

ODEMBA NI NANI?

Odemba ni mwanamitindo maarufu duniani aliyezaliwa Arusha mwaka 1983. Kabla ya kushiriki mashindano na maonesho makubwa mbalimbali ya urembo duniani, aliwahi kuwa Miss Temeke mwaka 1997. Mwaka 1998 alishiriki na kuingia kwenye kumi bora ya Shindano la Miss Tanzania kisha akaingia Tano Bora ya Shindano la M-Net Face of Africa. Pia mwaka 1999 aliingia kwenye 17 Bora ya Shindano la Elite Model Look Tanzania.

Related image

WAKATI HUOHUO…

Wakati huohuo, kuhusu Diamond na Wasafi wanatarajia kuanza ziara za lile tamasha lao kubwa la Wasafi Festival ambapo Jumamosi hii wataanzia kwenye Viwanja vya Nangwanda Sijaona mjini Iringa.

 

Kwa mujibu wa mmoja wa mameneja wa Wasafi, Babu Tale, Wasafi Festival itazunguka kwenye mikoa sita nchini ambapo maandalizi yake kwa kila mkoa ni zaidi ya shilingi milioni 200 hivyo kwa mikoa sita ni zaidi ya shilingi bilioni 1.2. Mbali na wasanii walio chini ya Wasafi, wapo wengine waalikwa ambao ni pamoja na Dudu Baya au Konki au Oil Chafu, Dully Sykes, Ibra Nation, Young Killer na Nikki Mbishi.

 

Wengine ni Khadija Kopa, Stereo, Moni Central Zone, Country Boy, Chin Beez, Orbit, One Incredible, Galatone na Navy Kenzo. Mbali na wasanii watakaoimba pia kutakuwa na watu maarufu ambao watakuwa nao kwa ajili ya kuchagiza burudani hizo ambao ni Kim Nana, Lemutuz, Official Nai, Tunda, Official Lynn, Jay Mond, Dully Van, Aunt Ezekiel, Steve Nyerere, Tausi, Asha Boko, Tabu Mtigita, Jacqueline Wolper, Kajala Masanja na wengine kibao.

WEMA Alivyotinga Mahakamani Tena, Kesi ya Video za Ngono!

Toa comment