The House of Favourite Newspapers

Mambo 6 usiyoyajua kuhusu… Yemi Alade

0

Yemi-Alade-

Yemi Alade

Machi 13, 1989 katika Jimbo la Abia nchini Nigeria alizaliwa staa wa muziki anayewakilisha Afrika kwa sasa, Yemi Eberechi Alade.
Miaka 16 baadaye, Yemi aliingia rasmi kwenye muziki ambapo alipofikisha miaka 20 tu alibuka kidedea katika shindano la kuibua vipaji vya kuimba lililojulikana kama Peak Talent Show.

Yemi hakukata tamaa, akiwa miaka 25, Tanzania ilimuona ambapo Agosti 8, ilikuwa historia kwake kukanyaga ardhi ya JPM na kufanya bonge moja la shoo katika Tamasha la Matumaini lililofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar kipindi hicho akibamba na Ngoma ya Johnny.

Leo hii, Yemi ni mmoja kati ya wanamuziki wa kike wenye nguvu zaidi barani Afrika kupitia muziki.
Katika makala haya yapo mambo 6 usiyoyajua kuhusu yeye;

1. Tangu aanze muziki, hadi sasa ana albamu mbili tu, ya kwanza inayoitwa King of Queens aliyoitoa mwaka 2014 na Mama Africa aliyoitoa wiki iliyopita.

2. Yemi ana mchanganyiko wa makabila mawili maarufu nchini Nigeria. Baba ni M-yoruba na mama ni M-igbo. Jina lake la katikati anaitwa Eberechi likimaanisha Mungu Mwenye Rehema.

3. Yemi havuti sigara lakini ni mnywaji wa pombe kali. Mara nyingi hutumia kilevi pale anapokosa usingizi.

4. Video ya Johnny imemfanya kuwa mwanamuziki wa kike na wa pekee nchini Nigeria kutazamwa na watu wengi (imetizamwa zaidi ya milioni 40 katika mtandao wa Youtube).

5. Anamiliki ‘application’ katika simu za kisasa za mkononi (smart phone)ambayo inaitwa Yemi Alade. Application hiyo imemfanya kuweka rekodi ya mwanamuziki pekee nchini Nigeria kumiliki.

6. Hadi sasa ana tuzo za saba na mbili za kimataifa ambazo ni kutoka MTV Africa Music (MAMA) na Black Entertainment Television (BET).

Leave A Reply