The House of Favourite Newspapers

Mambo Ya Kufanya Kwa Wanaotaka Kuingia Kwenye Ndoa!

0

WAUNGWANA mnaoishi kwenye maisha ya mahusiano nafurahi kukutana na nyinyi tena kwenye darasa hili zuri. Hapa ndipo tunapoelekezana, tunafundishana, tunapeana misingi ya kuishi vizuri kwenye maisha hususan ya mke na mume.Maisha ya mume na mke yana changamoto nyingi.

Mnakutana watu wawili ambao mmekutana ukubwani kila mtu ana kasumba zake. Hamuwezi kuwa sawa hata siku moja.

Wewe unaweza kuwa unapenda hiki ukiamini upo sahihi kumbe mwenzako hakipendi na kinamkwaza.Ndio maana mara kwa mara nimekuwa nikisema, maisha ya mahusiano yanahitaji uvumilivu. Yanahitaji hekima na busara ili kuwafanya muweze kuzivuka changamoto hizi za kutofautiana makuzi, malezi na tabia mbalimbali.

Ni kwa kutumia hekima ndipo mnaweza kuzun-gumza, kuelekeza-na na kukosoana kwa busara yale mambo ambayo si sahihi. Hauwezi kumb-dailisha mtu kwa kumfokea.

Huwezi kum-fokea mpenzi wako kama mtoto pindi anapofanya jambo ambalo si sahihi.Wapendanao wana namna yao rafiki ya kukosoana. Jipe nafasi ya kujifunza namna ya kumkosoa mwenza wako. Usikurupuke tu mathalan mpo kwenye hadhara wewe unamkosoa tu mwenza wako, kitakachokupata utakuwa unastahili.Usishangae kuona unapewa tusi zito au kugeuziwa kibao kwa sababu tu, hukutumia busara.

Ulipaswa kutafuta namna ya kumtoa pembeni mwenza wako na kumueleza kile ambacho wewe unaamini kilikuwa sahihi na sio kuropoka mbele za watu.Ndugu zangu hizo busara na hekima za kuzungumza tutakuja kuzijadili siku nyingine lakini leo nataka kuzungumza na wale ambao mnataka kuingia kwenye ndoa.

Wale ambao mnatamani kuyaacha maisha ya ubachela na muingie kwenye udugu wa mke na mume.Wengi wetu tumekuwa tukikosea suala hili kwa kulifanya kama la kawaida tu hivi. Tunaingia kwenye ndoa kama vile jambo la majaribio hivi, kwamba upo uwezekano kesho na keshokutwa ukaachana nayo ndoa na maisha yakaendelea.

Ndugu zangu tunakosea sana. Unapotaka kuingia kwenye ndoa hakikisha kweli unamaanisha kwamba unajua misingi yake na sasa upo tayari kuingia kwenye kundi hilo. Usiingie tu kwa kushinikizwa na watu au kuona lab-da umri umeen-da hivyo na wewe uoe au uolewe.

Ingia kwenye ndoa ukiwa ni wakati sahihi ambao wewe umeuona unafaa kwa kushirikiana na mwenza wako ambaye naye atakuwa tayari kweli kuingia kwenye maisha hayo. Usilazimishe ndoa wakati mwenzako hayupo tayari.

Jitahidi sana kumshirikisha mwenzako kwenye wazo hilo, akubaliane nalo na ndipo muamue kwa pamoja kwamba mnaingia kwenye jambo hilo lini na kwa njia gani. Ninaposema kwa njia gani, ndoa inahitaji maandalizi.Kwa wale Wakristo watanielewa zaidi lakini hata Waislamu pia hili linawafaa.

Nyinyi ndio wahusika wakuu, kama ni muvi nyinyi ndio ‘masteringi’ hivyo lazima mkubaliane kwanza mnaingia kwenye ndoa ya aina gani?

JE, MNATAKA NDOA KU-FUNGA NDOA YA WATU WENGI AU WACHACHE? Mnataka harusi iwe kubwa, wastani au ndogo? Ili muweze kufikia hilo mna-takiwa kujitathini. Kwamba nyinyi ni watu wa ndoa ipi? Mkishajifahamu basi mfunge ndoa yenu.Msilazimishe kufunga ndoa ambayo si saizi yenu.

Itawagharimu bure kung’ang’ania maisha ambayo si yenu, nyinyi mnapaswa kuishi nyinyi kama nyinyi. Hakuna sababu ya kuumiza kichwa kushindana na mtu au kulazimishwa na mtu.Asiwepo mtu wa ku-washikia akili kwamba ili mheshimike mfunge ndoa ya aina hii au hii, hiyo sio yao ni ndoa yenu.

Fungeni ile mnayoamini mnaimudu. Hiyo wanayowashauri waambieni waifunge wao. Hakuna sababu ya kujiumiza kwa madeni ili tu kujitengen-ezea sifa ya siku moja.Ndugu zangu, ndoa ni ya kwenu. Chagueni ile ambayo mnaona nyinyi inawafaa.

Hakuna kiongozi wa dini atakaowacheka eti kwa nini mmefunga ndoa bila kula pilau na kuwa na ukumbi mkubwa.

Viongozi wa dini wanatamani nyinyi mfanye tendo hilo takatifu kanisani hayo mengine ni ziada tu.Mnaweza mkafunga ndoa na mkanywa soda zenu na maji kidogo maisha yakaendelea. Nyinyi kwenye akili yenu ndio mnajua umuhimu wa tendo hilo. Mmeshalikamilisha basi mumshukuru Mungu kwani hizo fedha zinatafutwa.Kama mnataka kufanya sherehe mbona zipo tu mtazifanya sana.

Siku hizi kuna watu wanafanya sherehe ya bethidei kubwa kuliko harusi ukifuatilia kwa makini unaweza kukuta mtu wa aina hiyo hakufanya sherehe kubwa kwenye harusi yake hivyo ameamua kufanya tukio hilo kuwa kubwa kama sehemu ya kujifurahisha.

Sio lazima bethidei tu, mnaweza tu kuamua siku mko vizuri na mkajifanyia bonge la sherehe wewe na familia yako hivyo mambo haya yasiwaumize kichwa.

Leave A Reply