The House of Favourite Newspapers

GUARDIOLA NA KIKOSI CHA UBINGWA ENGLAND

0
Kocha wa timu ya Man city, Pep Guardiola akiongea na wachezaji wake hawapo pichani.

City ni kati ya timu ambayo msimu uliopita ilishindwa kufanya vizuri pamoja na kwamba ilikuwa chini ya kocha mahiri, Pep Guardiola. Awali kabla msimu haujaanza mashabiki wengi waliipa timu hii nafasi kubwa ya kufanya vizuri kutokana na maandalizi na usajili ambao walikuwa wameufanya lakini mwisho wa msimu timu hiyo ilimaliza ikiwa katika nafasi ya tatu kwenye ligi. Haya hayakuwa mafanikio kwa timu hiyo kwani ilikuwa imefanya maandalizi mazuri sana kuhakikisha kuwa inamaliza vizuri msimu huo.

Lakini ilijikutaka ikipoteza kombe moja baada ya lingine na mwisho wa msimu Guardiola alisema kuwa timu yake haikuwa imara kwa ajili ya kutwaa makombe na kuwapa mashabiki wa timu hiyo ahadi mpya.

“Hatukuwa vizuri, baadhi ya wachezaji hawakujituma vyema jambo ambalo limetufanya tumalize msimu vibaya, kupata nafasi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya siyo mafanikio kwetu, tulitakiwa kutwaa ubingwa wa England au Ligi ya Mabingwa Ulaya, hiyo ndiyo ilikuwa ahadi yetu “Lakini napenda kuwaahidi mashabiki wa City kuwa tutarejea msimu ujao tukiwa na nguvu kubwa zaidi, kasi zaidi na najua kuwa kama hatutatwaa ubingwa basi City hawawezi kuniacha niendelee kuwa hapa,” alisema Guardiola mwishoni mwa msimu uliopita.

Kikosi cha Man City.

Kweli kocha huyo ameanza kuonyesha makeke yake kwenye usajili kwani kati ya timu ambayo imefanya usajili kabambe msimu huu hadi sasa basi Man City ni mojawapo. Timu hii inayotumia Uwanja wa Etihad imefanya usajili wa wachezaji wengi sana bora ikiwa na nia moja tu ya kuhakikisha kuwa inatwaa ubingwa wa Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Hadi sasa timu hiyo imeshafanikiwa kusajili wachezaji watano wakubwa, hii ikiwa na maana kuwa kuna mastaa watano aidha watauzwa au watakosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha City msimu ujao. Usajili wa mwisho kufanywa na kocha huyo ni wa Mbrazil, Danilo, ambaye amejiunga na timu hiyo akitokea Real Madrid ya Hispania. Danilo, ambaye amekuwa akiwindwa na Guardiola kwa muda

 

mrefu anaaminika kuwa atakuwa msaada mkubwa kwa kocha huyo kwenye safu ya ulinzi ambayo msimu uliopita ilikuwa ikitetereka kwenye kila mchezo. Beki huyo amesajiliwa kwa kitita cha pauni milioni 27, zaidi ya shilingi bilioni 76, na kuwa mchezaji wa tano kujiunga na timu hiyo ya England.

 

Alipomaliza kujiunga na timu hiyo beki huyo alise- ma kuwa anajua shida ya Manchester City na atajitahidi kufanya kila jambo kuhakikishawanakuwa na msimu mzuri. Hata hivyo, kumekuwa na hofu kubwa sana kut o k a n a na jinsi Guardiola anavyofanya usajili wake kwani wengi wameanza kupata hofu ya kutokujua nini ambacho kocha huyo anataka kukifanya baada pia kumsajili beki Benjamin Mendy, ambaye naye anacheza kama beki wa pembeni na huyu anakuwa mchezaji wa tatu wa timu hiyo kusajiliwa kwenye nafasi hiyo. Hii ina maana kuwa Guardiola atakuwa ametumia kitita cha pauni milioni 133 zaidi ya shilingi bilioni 378, kwa mabeki watatu wa pembeni.

 

Lakini kuonyesha kuwa k o c h a h u y o hataki kufanya mzaha kwa msimu ujao tayari jumla ameshatumia kitita cha pauni milioni 221, kwa ajili ya kuunda kikosi kipya cha City. Danilo, ni mzuri zaidi akicheza kama beki wa kushoto, huku pia timu hiyo ikiwa na Walker ambaye amekuwa bora zaidi kwenye u p a n d e wa kulia, ambao na Benjamin Mendy ambaye atawapa upinzani kwenye nafasi hio.

 

Hata hivyo, usajili huu wa Guardiola ambao unaonekana kuungwa mkono na mabosi wa timu hiyo ni dhahiri kuwa wanataka timu hiyo ifanye v i z u r i k w a ajili ya msimu ujao. “Usajili wa Danilo, ni usajili sahihi kwenye timu hii, tunaamini kuwa atafanya vizuri na hilo ndiyo litakuwa jambo zuri kwetu, ni mchezaji mzuri ambaye amek u w a akionyesha kiwango bora sana uwanjani. “Anaweza kucheza kwenye nafasi nyingi uwanjani, anaweza kucheza kama beki na wakati mwingine kama kiungo hawa ni wachezaji wachache sana duniani.

 

“Lakini pia nipongeze kwa kila mchezaji ambaye amejiunga na timu hii, naamini kila mmoja ataonyesha kiwango cha juu kuhakikisha kuwa timu hii inapata mafanikio msimu u j a o , ” anasema Mkurugenzi wa timu hiyo, Txiki Begiristain. Pamoja na kufanya usajili huo, City imeachana na wachezaji watatu mahiri Bacary Sagna, Gael Clichy na Pablo Zabaleta, ambao wameondoka kwenye timu hiyo na hawa wote walikuwa wakicheza kwenye nafasi ya mabeki wa pembeni. Hata hivyo, tayari timu hiyo inatafuta timu kwa ajili ya kuwapeleka wachezaji wawili kwa mkopo, Kelechi Iheanacho na Wilfried Bony. Wachezaji wote wawili hawakuwa kwenye ziara ya timu hiyo ya nchini Marekani, huku klabu ya Swansea ikitajwa kuwa inataka kumsajili Bony a m b a y e aligoma kujiunga na timu mbalimbali za nchini China ambazo zilikuwa zikihitaji huduma yake.

 

Leave A Reply