Man United Yapata Pigo
KIUNGO wa kati wa Manchester United Paul Pogba hatoshiriki katika mechi ya michuano ya kufuzu kwa kombe la dunia baada ya kupata jeraha la nyonga.
Mshindi huyo wa Kombe la Dunia, mwenye umri wa miaka 28 alipata jeraha wakati wa mazoezi jana Jumatatu , Shirikisho la soka nchini Ufaransa FFF limesema.
Pogba hatoshiriki katika mechi ya Jumamosi dhidi ya Kazakhstan ama mechi ya ugenini dhidi ya Finland Novemba 16.
Tayari alitarajiwa kukosa mechi ya United ugenini dhidi ya Watford katika ligi ya Premia tarehe 20 Novemba , huku akikamilisha marafuku yake ya mechi tatu.
Pogba alipokea marufuku hiyo kabla ya kutolewa nje wakati wamechi ya kichapo cha 5-0 dhidi ya Liverpool tarehe 24 mwezi Oktoba.