The House of Favourite Newspapers

Man Utd Yamchoka Pogba, Kuuzwa Bei Chee

0

KLABU ya Manchester United ni wazi kuwa imechoshwa na mwenendo wa matukio yanayomuhusu kiungo wao, Paul Pogba na sasa wapo tayari kumuuza katika dirisha dogo la mwezi ujao.

 

Imeelezwa taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo kuwa wameona ni bora wamuuze katika usajili wa Januari kwa bei ndogo kuliko kusubiri mwisho wa msimu kumuuza kwa dau kubwa kama walivyokuwa wakitaka awali.

 

Pogba amegusa vyombo vya habari mara baada ya wakala wake, Mino Raiola kunukuliwa akisema maneno kadhaa kuhusu United na kudai mteja wake hana furaha.

Mbali na hapo alitoa kauli nyingine mbaya kwa kocha wa United muda mfupi kabla ya timu hiyo kutolewa katika Uefa Champions League kwa kufungwa dhidi ya RB Leipzig mabao 3-2, Jumanne iliyopita.

 

Hivyo, Manchester United ipo tayari kumuuza hata kwa euro 55m badala ya euro 100m na zaidi kama walivyokuwa wakitaka awali.Awali Pogba alikuwa akiwaniwa kwa ukaribu na Real Madrid lakini inaonekana wazi njia yake ni nyeupe kwenda Juventus

Leave A Reply