The House of Favourite Newspapers

Manara Aponda Usajili wa Tuisila na Mukoko Tonombe -Video

0


HAJI Manara, Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa anawapenda mashabiki wa Yanga kwa kuwa ni wavumilivu ila kitendo cha kumbeba kiongozi wao juu ni tukio la hovyo.

Jana Agosti 20, Yanga waliwapokea wachezaji wake wapya wawili ambao ni Tuisila Kisinda na Tonombe Mukoko wote kutoka AS Vita na kwenye mapokezi hayo Injinia Hersi Said ambaye ni Mkurugenzi Mwekezaji kutoka Kampuni ya GSM alibebwa juu mithili ya mfalme.

Manara amesema:-“Kaangalie line up ya AS Vita ya mwaka jana hadi sasa uone kama hao wachezaji waliowasajili walikuwepo. AS Vita wanacheza Champions League kama wanamuhitaji mchezaji unadhani wanaweza kumuacha kirahisi aondoke?

“Yanga baada ya kuondoka kwa Manji wametetereka, hawatakiwi kujitutumua pale walipo ili washindane na Simba, wakubali kurudi nyuma wajipange. Msimu uliopita walisajili wachezaji 25, haijawahi kutokea hii!” amesema Manara

Manara ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na kituo cha +255 Global Radio ambapo amesema kuwa anaamini mashabiki wa Yanga ni wavumilivu.

” Kitu pekee ambacho nakipenda Yanga ni kuwa wana moyo wa chuma, ni wavumilivu hasa, kwa matokeo yale wanayopata huku wanambeba kiongozi wao juu, ni tukio la hovyo kabisa lile.”

Leave A Reply