The House of Favourite Newspapers

Manara Atoa Jezi Tandale, Kuanzisha Ligi ya Diamond (Picha + Video)

Afisa habari wa Simba Haji Manara katika Uwanja wa Magunia Tandale jijini Dar es Salaam  katika kuadhimisha kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

MSEMAJI wa Klabu ya Simba, Haji Manara leo ameungana na viongozi mbalimbali wa serikali, warfanyabiashara na wasanii kumuunga mkono msanii Diamond Platnums kwenye sherehe yake ya kuzaliwa iliyofanyika nyumbani kwao, Tandale Maguniani.

 

Katika tukio hilo ambapo Diamond ametoa Bajaj kwa mlemavu Bi. Evodia Nchimbi wa Mburahati, pikipiki 20 kwa vijana wa Tandale, bima za afya kwa watoto 1,000, mitaji kwa akina mama na vijana, Haji Manara aliufananisha umati uliofika kumuona nyota huyo na wapiga kura kwa kusema Diamond angepita bila kupingwa iwapo angegombea nafasi yoyote ya ubunge.

Haji Manara akiongea na Umati wa mashabiki wa Diamond (hawapo pichani) walifika katika Uwanja wa Magunia.

“Kama Diamond angetaka kufanya siasa hizi zote kura zake nawaambia, nimejaribu kumuuliza kuhusu hilo lakini mwenyewe amesema hataki kufanya siasa hivyo wanasiasa mtulize roho zenu,” amesema Manara.

Mara baada ya kusema hayo shangwe ziliibuka uwanjani hapo na baadaye Manara alizungumza tena na baadaye alitoa mipira kwa shule za Tandale.

Diamond Platnumz akikabidhiwa jezi na Haji Manara kwa ajili ya shule za Tandale.

Amesema ili watoto wakue vizuri ni muhimu wapate muda wa kucheza hivyo anatoa mipira hiyo ili kuhakikisha wanashiriki michezo.

Amesema katika kumuunga mkono Diamond amezungumza na wadau ambao wamekubali kuweka ligi Tandale itakayofahamika kwa jina la ‘Diamond Tandale Super Cup.’

Makabidhiano yakiendelea.

Manara ametangaza kugharamia ada za wanafunzi wote walemavu watakaoanza shule Januari mwakani.

“Wanafunzi walemavu wote watakaoanza mwakani nitalipa ada kuanzia msingi hadi sekondari ili mradi iwe shule za serikali,” amesema Manara huku akishangiliwa.

Haji Manara akimkabidhi Diamond Platnumz (kushoto) mpira kwa ajili ya shule za Tandale.

 

PICHA: RICHARD BUKOS, GPL

Comments are closed.