The House of Favourite Newspapers

Manchester City Yamalizana na Dias wa Benfica

0

KLABU ya Manchester City imekubali kumsajili beki Ruben Dias kwa kitita cha pauni milioni 65 zaidi ya shilingi bilioni 192, kutoka Benfica ya Ureno.

City wamekuwa wakilalamika kuanzia msimu uliopita kuwa safu yao ya ulinzi haipo vizuri na sasa wanataka kuhakikisha kuwa wanakuwa bora.

Walishindwa kufanya mambo makubwa kwenye mchezo wa wikiendi iliyopita dhidi ya Leicester City ambapo walichapwa mabao 5-2 kwenye Ligi Kuu England.

 

Makubaliano ya City na timu hiyo ni kwamba wakishampata mchezaji huyo wanatakiwa kumuachia beki wa Nicolas Otamendi kujiunga na Benfica.

Taarifa iliyotolewa na klabu ya Benfica inasema kuwa wameshakubaliana kila kitu na Man City na mchezaji huyo msimu huu atakuwa mali ya City.

 

“Kinachosubiriwa ni mambo madogo tu ya kukamilisha dili hilo, lakini kama klabu zote mbili tumesha kubaliana kuwa Dias anakwenda Man City, tunasikitika kumuachia kwa kuwa ni mchezaji wetu kuanzia akiwa kijana,” ilisema taarifa hiyo

Leave A Reply