The House of Favourite Newspapers

Manchester United Yamtengea Aubameyang Bilioni 132

0

KLABU ya Manchester United inajiandaa kutoa pauni milioni 50 (Sh bil 132) kwa ajili ya kufanikisha mpango wa kumsajili straika wa Arsenal, Pierre Emerick Aubameyang. Imeelezwa kuwa Arsenal inaweza kumuweka sokoni mshambuliaji huyo ambaye mkataba wake unamalizika mwakani na hajasaini mkataba mpya hadi sasa.

 

Kumekuwa na mvutano mkali ndani ya Arsenal kuhusu mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30, kama wamuuze au wamruhusu aondoke bure pindi mkataba wake utakapomalizika. Mvutano huo unataka kutumiwa vizuri na Kocha wa Man United, Ole Gunnar Solskjaer ili amsajili na kuboresha kikosi chake.

Aubameyang amekuwa akitajwa kuwa yupo njiani kuondoka klabuni hapo, licha ya kuwa kocha wake, Mikel Arteta amekuwa akihitaji kuendelea kuwa naye.  Arsenal waliilipa Borussia Dortmund pauni 56m ili kumsajili Januari 2018, na kuwa mchezaji aliyesajiliwa kwa dau kubwa zaidi klabuni hapo wakati huo, bado inahitaji kuendelea kuwa naye lakini bado mwenyewe hajaonyesha nia ya kubaki hapo.

 

Mbali na United, pia klabu za Barcelona na Paris SaintGermain zote zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili. Manchester United ilimsajili Odion Ighalo kwa mkopo akitokea Shanghai Shenhua ya China, Januari, mwaka huu baada ya kushindwa kumsajili straika wa Bournemouth, Josh King. Ighalo amekuwa na mwanzo mzuri tangu asajiliwe lakini kuna uwezekanao wa kuhitajika straika mwingine ili kuongeza nguvu msimu ujao

 

Leave A Reply