The House of Favourite Newspapers

MANCHESTER UNITED YASHINDA, LUKAKU ATUPIA APOTEZEA KUSHANGILIA

Wachezaji wa Manchester United.

Manchester United haijakata tamaa katika kuifukuzia Manchester City kwenye mbio za ubingwa wa Premier League baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1.

Ushindi huo unaifanya Man United kupunguza pointi kati yao na Man City kwa kuwa pointi 11 badala ya 14 kama ilivyokuwa awali baada ya Man City kuifunga Tottenham Hotspur, juzi.

Mabao ya Manchester United yaliwekwa wavuni na Romelu Lukaku dakika ya 35 na Jesse Lingard dakika ya 53, wakati lile la West Bromwich Albion liliwekwa wavuni na Gareth Barry katika dakika ya 77.

Mara baada ya kufunga Lukaku hakushangilia kama ilivyokuwa katika mchezo uliopita dhidi ya AFC Bournemouth ambapo alifunga na hakushangilia.

Comments are closed.