The House of Favourite Newspapers

Manchester yatumbuliwa na Liverpool

0

1

Coutinho akishangilia na wachezaji wenzake wa Liverpool baada ya kusawazishia bao dhidi ya Manchester United dakika ya 45 ya mchezo.3

Kinda wa Man United, Marcus Rashford (kushoto) akijaribu kumtoka Mamadou Sakho wa Liverpool wakati wa mechi hiyo.

2

Kipa wa Manchester United, De Gea akiangalia mpira uliopigwa na Coutinho ukielekea nyavuni.

4

Kiungo wa Liverpool, Adam Lallana akijaribu kumchomoka Jesse Lingard wa Manchester United (kulia).

LIVERPOOL imetinga robo fainali ya michuano ya Europa League baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Manchester United katika mchezo wa marudiano wa 16 Bora, jana usiku kwenye Uwanja wa Old Trafford.

Ikiwa chini ya Kocha Jurgen Klopp, Liverpool imesonga mbele kwa jumla ya mabao 3-1 baada ya kushinda mabao 2-0 katika mchezo wa awali.

Katika mchezo wa jana, Man United ikicheza nyumbani ilikuwa ya kwanza kupata bao kwa njia ya penalti dakika ya 32 kupita kwa Anthony Martial.

Penalti hiyo ilipatikana baada ya Nathaniel Clyne wa Liverpool kumuangusha Martial ndani ya eneo la hatari.

Baada ya bao hilo, Liverpool ilipambana na kusawazisha dakika ya 45 kupitia kwa Philippe Coutinho aliyepokea pasi ya Emre Can kisha kumtoka beki wa Man United, Guillermo Varela na kufunga.

Kipindi cha pili Man United ilimtoa Varela na kumuingiza Antonio Valencia, pia akatoka Michael Carrick na kuingia Bastian Schweinsteiger huku Liverpool ikiwatoa Daniel Sturridge na Jordan Henderson na kuwaingiza Divock Okoth na Joe Allen.

Matokeo mengine ya mechi za jana usiku katika michuano hiyo; Bayer Leverkusen 0-0 Villarreal, Lazio 0-3 Sparta Prague, Valencia 2-1 Athletic Bilbao, Anderlecht 0-1 Shakhtar Donetsk, Braga 4-1 Fenerbahce, Sevilla 3-0 Basel, Tottenham Hotspur 1-2 Borussia Dortmund.

Leave A Reply