The House of Favourite Newspapers

Manji Hali ni Tete, Azidi Kusota Mahabusu

0
Manji akitoka kwenye lango la Mahakama Kuu.

 

Upande wa serikali umewasilisha pingamizi la awali Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga maombi ya dhamana ya mfanyabiashara Yusuf Manji.

 

…Akienda kupanda kwenye gari ili arudishwe Gereza la Keko.

 

Pingamizi hilo limewasilishwa leo na wakili wa serikali, Paul Kadushi mbele ya Naibu Msajili, Sian Mustafa kutokana na Jaji Isaya Arufan anayesikiliza maombi hayo kutokuwepo.

 

Katika pingamizi hilo, wakili Kadushi amedai kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza maombi ya dhamana ya Manji.

Pia kiapo kilichowasilisha cha kuhusu dhamana kinadosari kisheria, pamoja na kuwepo kwa vifungu visivyo sahihi.

Muonekano wa Manji wa sasa.

 

Baada ya kuwasilisha pingamizi hilo, Msajili Mustafa ameahirisha kesi hiyo hadi August 7/2017 kwa ajili ya kusikilizwa.

 

Julai 5 mwaka huu, akiwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Manji alisomewa mashtaka saba na watuhumiwa wenzake, yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na wa Commanding Officer Korogwe, plate number mbili za magari ya serikali jambo ambalo nalo ni kinyume cha sheria.

 

Watuhumiwa wengine katika sakata hilo ni Deogratius Kasinda na Thobias Pwere na mwingine ambaye jina lake halikufahamika mara moja na wote wamerudishwa rumande.

Leave A Reply