The House of Favourite Newspapers

Manji Mikononi mwa Takukuru, Sababu Zatajwa

0

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imethibitisha kuwa inamshikilia mfanyabiashara Yusuph Manji kwa mahojiano.

Manji, ambaye aliondoka nchini mwaka 2018 baada ya Serikali kuondoa nia ya kuendelea na kesi iliyokuwa ikimkabili, amerejea juzi jioni na baada ya kukamilisha taratibu za uhamiaji akachukuliwa na maofisa wa Takukuru.

Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Kamishna wa Polisi Salum Hamduni amesema kuwa wanamshikilia Manji kutokana na tuhuma tatu zinazomkabili.

Hamduni amesema kabla ya Manji kutoroka nchini kuna uchunguzi ulifanywa kuhusu kampuni zake za Intertrade Commercial Ltd Services na Golden Globe International Services Limited.

Leave A Reply