The House of Favourite Newspapers

Maombi Yaliyowasilishwa Mahakama Kuu na Chama cha Ushirika Uduru Makoa Uamuzi Agost 16

0
Jopo la mawakili wa upande wa wajibu maombi wakiteta jambo.

 

BAADA ya mawasilisho ya maombi madogo ambayo yaliyowasilishwa  Mahakama Kuu Kanda ya Moshi na Chama cha Ushirika Uduru Makoa dhidi ya mwekezaji Makoa Farm yamepangwa kutolewa uamuzi Agost 16 mwaka huu.

 

Awali vuguvugu la mgogoro huo dhidi ya mwekezaji, Elizabert raia wa Ujerumani mwenye mkataba wa miaka 35 katika shamba hilo la makoa lenye takribani Hekari 368 lililopo wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro ulianza takribani miezi mitano imepita sasa lakini ulichachamaa na kufikishwa mahakamani hapo wiki tatu zilizopita huku mwekezaji huyo akidaiwa kuvunja masharti ya mkataba wake ikiwemo kubadilisha matumizi ya ardhi na kutokutoa ajira kwa wananchi wa eneo hilo.

Wanachama wa Chama cha Uduru wakiwa mahakamani kufuatilia mwenendo wa kesi yao.

 

Kwa mara ya kwanza shauri hilo limesikilizwa hii leo baada ya mawakili wote wa pande mbili kuwasilisha maoni yao. Akiongea na waandishi wa habari wakili wa Makoa Farm Henry Masaba amesema kuwa tayari wametoa hoja kuhusiana na kile ambacho mtoa maombi anawalalamikia na kuwa baada ya jaji kusikiliza pande zote amepanga tarehe hiyo kutoa uamuzi.

Wanachama wa Chama cha Ushirika Uduru wakifuatilia kesi hiyo kiumakini.

 

Amesema uamuzi huo ndio utakaoamua kuwa kesi ya msingi namba 4 ya mwaka 2022 iendelee au kama wataweka mapingamizi mengine itashindwa kuendelea. Kwa upande wake wakili wa upande wa watoa maombi ambao ni chama cha ushirika Uduru Egberth Boniface kuwa baada ya mabishano ya kisheria sasa tarehe 16 ndipo uamuzi utaenda kutolewa na jaji na kuwa atakuja na mapingamizi mengine.

Mawakili wa waleta maombi wakijiandaa kuwasilisha maombi mbele ya mahakama.

 

Jaji Thadeo Mwenempazi ndiye aliyekuwa akisikiliza maombi hayo na kuwa tayari baada ya kusikiliza pande zote amepanga kutoa maamuzi tarehe 16 mwezi huu.

 HABARI/PICHA NA ISAACK MAKOI, KILIMANJARO

Leave A Reply