The House of Favourite Newspapers

Mapazia ya chumbani -15

0

ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:
“Hee makubwa!”
Aliropoka mama Muro baada ya kuliangalia lile jina.
“Kwa hiyo hakuna kulemba, tunataka na meseji ya kwanza umtumie tukiwa wote hapa,” alisema mama Dick.
ENDELEA NAYO MWENYEWE…
“Nyie ndiyo mnajua mchezo mzima jinsi ya kumuingilia huyu maza mnayemsema, sasa nitaanza kuandika meseji gani, niambieni,” alihoji yule kijana.
“Embu lete hiyo simu,” alisema mama Muro na kuchukua ile simu kisha akaandika.
‘Mpenzi vipi umeshalala?’
Kisha baada ya hapo wakaituma na kujificha ili mama Kirumba asije kutoka ndani kwake ghafla mambo yakaharibika.
Haikuchukua muda meseji ile ikajibiwa.
‘Nilale wapi hofu kwako tu.’
Mama Muro na mama Dick baada ya kuisoma meseji ile moyoni walifarijika sana badala ya kukasirika.
“Kazi imekwisha!” walijikuta wakiongea kwa pamoja.
“Sasa mambo mengine utaendelea nayo,” alisema mama Muro.
“Sisi hapa wala hatubanduki tuko nyuma yako, utakuwa unatujulisha kwa kila kinachoendelea ili tuumalize mtego wetu vizuri,” alidakia mama Dick.
Yule kijana alijikongoja hadi kwenye ukuta wa nyumba ya mama Kirumba kisha akatuma meseji.
‘Mpenzi nahitaji tufanye tena ule mchezo.’
Akasubiri ndani ya dakika chache majibu yakaja. ‘Nakusikiliza wewe tu, mkeo si yupo?’
‘Yupo lakini ameshalala zake, nipo kitandani usingizi sina si unajua nyumba zetu hizi, nasikia joto tupu.’
Yule kijana alikuwa mtaalam wa kucheza na akili ya mama Kirumba. Mama Kirumba hakutambua lolote juu ya meseji alizokuwa anajibishana na ile namba. Alijua moja kwa moja ni mzee Mashali kutokana na namba aliyokuwa nayo.
‘Kama joto ujue na huku kwangu joto hivyohivyo, njoo basi tulale wote sakafuni,’ aliandika mama Kirumba na kumfanya yule kijana kuzidiwa na mzuka.
Alichokifanya ni kumchanganya zaidi mama Kirumba kwa meseji kisha akawatumia meseji kina mama Muro.
‘Ameshalainika, muda si mrefu nitakua ndani ya nyumba yake, nitahakikisha mlango wake upo wazi hadi chumbani,’ aliandika yule kijana kisha akawatumie mama Muro na mwenzake, wakaipokea.
“Shosti! Amekwisha!” alisema mama Dick kwa furaha baada ya kuisoma ile meseji.
“Siyo tu amekwisha, litamshuka leo, kumbe anajifanya hana mchumba wala mume, mara ohh alizalishagwa akaachwa, leo ataisoma namba mbona! Halooo!!!” alisema mama Muro huku akiangua kicheko cha kimbeya.

***
Yule kijana mbali na kutumia namba ya mzee Mashali kama mtego wa kumkamatisha mama Kirumba, pia alikuwa ameshanogewa kwa meseji alizokuwa akitumiana na mama Kirumba.
“Sicheleweshi lazima, ngoja nimuweke kwanza kati,” alijisemea kisha akatuma meseji nyingine.
‘Unasema nije tulale wote.’
‘Ndiyo tena sakafuni mpenzi tunapata na mambo yetu yale.’
Yule kijana hakuamini macho yake, mzuka ulimzidia mara mbili yake, akatuma tena meseji.
‘Natoka basi, lakini nihakikishie kitu kimoja mpenzi.’
‘Kitu gani tena!’
‘Nataka uzime taa ili mke wangu asigundue!’
‘Hilo usijali nazima mpaka ya nje, we njoo tu moja kwa moja utanikuta chumbani au unataka nitoke hadi sebuleni?’ aliandika mama Kirumba.
‘Hata sebuleni itakuwa sawa, ila kwanza nikukute umejiweka sawa nikifika tu tunaanza.’
Yule kijana hakutaka kupoteza muda, macho yake yalikuwa hayatoki kwenye taa za nyumba ile ya mama Kirumba. Aliamini ndani ya muda mfupi taa zingezimwa na kweli zoezi hilo likafanyika. Kwa ujasiri alichokifanya ni kupiga hatua moja kwa moja hadi mlangoni.
Akashika kitasa na kufungua, mlango kweli ulikuwa haujafungwa.
“Karibu nipo kwa huku,” ilisikika sauti taratibu kama ya mtu anayenong’oneza, alikuwa ni mama Kirumba na kwa urefu wa yule kijana alishajua ni kweli mzee Mashali.
Alichokifanya mama Kirumba ni kujihakikishia kwa mara nyingine kwa kutumia ile namba ya mzee Mashali, akapiga kama simu ataisikia ikiita. Akafanya hivyo simu ikaita, akaikata.
“Njoo kwa huku mpenzi,” alisema mama Kirumba.
Muda wote yule kijana hakutaka kuongea chochote alijua endapo sauti yake ikisikika atagundulika kirahisi. Alichokifanya ni kusogea kimyakimya kisha akaanza kuushika mwili wa mama Kirumba kwa hisia zote.
“Mpenzi tuanze basi,” alisema mama Kirumba.
Maneno yale yalimkuna yule kijana, alichokifanya alivua nguo zote kisha akachukua simu na kutuma meseji kwa mama Muro na mwenzake.
‘Njooni hadi sebuleni mlango upo wazi!’

Je, nini kiliendelea hapo? Usikose chombezo hili wiki ijayo.

Leave A Reply