The House of Favourite Newspapers

Mapenzi Yamficha Masogange

0

VIDEO Queen mwenye figa bomba Bongo, Agnes Jerald ‘Masogange’ amefunguka kuwa ukimya wake wa hivi karibuni na kutojichanganya kwa watu mbalimbali ni kwa sababu ya mpenzi ambaye amempata kwa sasa kwani anambana sana.

 

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Masogange alisema hivi sasa haendi sehemu yoyote ya starehe wala kujichanganya na watu wengi kwa sababu mpenzi wake huyo amempa masharti hayo na yeye ni lazima ayafuate kwani anaheshimu penzi lake.

 

“Unajua kipindi cha nyuma kilikuwa cha utoto zaidi kwa sasa nimejitambua vizuri zaidi na ukiwa na mtu ambaye anakusaidia akawa hataki vitu fulani ni lazima kuheshimu ndiyo maana sionekani ovyo kwa sasa,” alisema Masogange.

 

STORI: IMELDA MTEMA | RISASI VIBES

 

Mkali wao Atoboa siri nzito, Heeee!!!!! Kumbe Ebitoke Kumtaka Benpol ilikuwa ni kiki???

Leave A Reply