The House of Favourite Newspapers

Mary Mawigi Aumizwa na Jini Kabula

0
Mary Mawigi

 

MSANII wa filamu za Kibongo, Mary Mawigi ameeleza kuumizwa kwake na msanii mwenzake ambaye alikuwa rafiki yake pia, Miriamu Jolwa ‘Jini Kabula’ kuchanganyikiwa na kuwaomba Watanzania wamuombee.

 

Akipiga stori na Risasi Jumamosi, Mary alisema hali aliyonayo Jini Kabula inaumiza na inaweza kumkuta mtu yeyote hivyo kwa kipindi hiki ushirikiano unatakiwa kuwa mkubwa kwa familia yake ili aweze kupata gharama za matibabu pamoja na ushauri.

Jini Kabula

 

“Nimeumizwa sana na hali ya Kabula ila namuombea Mungu amsaidie ili aweze kupona na kurudi katika hali yake ya kawaida maombi haya yasiishie kwangu naomba hata mashabiki zetu wamuombee kwani anahitaji maombi zaidi ili arudi kwenye hali ya kawaida,” alisema Mawigi.

 

STORI: GLADNESS MALLYA | RIASAI MCHANGANYIKO

Stamina, Darassa Kulipeleka Jiji Dar Live Sikukuu ya Idd Mosi

Leave A Reply