The House of Favourite Newspapers

Mapigano Makali Ukraine, Bomba la Gesi Lalipuka

0

Mji Mkuu wa Ukraine, Kyiv umekabiliwa na mashambulio makali ya Urusi usiku wa kuamkia leo Februari 27, 2022. Wakati huohuo, mataifa ya Magharibi yanapanga kuziondoa baadhi za benki za Urusi kutoka kwenye mfumo wa fedha wa kimataifa (SWIFT).

 

Taarifa ya Jeshi la Ukraine imesema kuwa wanajeshi hao wa Urusi pia wanakabiliwa na upinzani mkubwa ikiwa ni pamoja na vikosi hivyo vya Ukraine kuzuia shambulio la Urusi karibu na Mji wa Kharkiv uliopo Kaskazini Mashariki mwa Ukraine.

 

Ofisi ya Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy imesema kumetokea mlipuko kwenye bomba la gesi, Kusini mwa mji mkuu wa Kyiv mapema Jumapili. Amri ya kutotoka nje imewekwa katika mji huo mkuu wa hadi kesho Jumatatu.

 

Katika hatua nyingine, Balozi wa Ukraine nchini Ujerumani, Andrij Melnyk ameelezea furaha yake kutokana na uamuzi wa Ujerumani wa kupeleka silaha nchini Ukraine. Balozi huyo ameliambia Shirika la Habari la Ujerumani (DPA) kuwa hatua hiyo ni ya kihistoria.

Leave A Reply