The House of Favourite Newspapers

Watu 14 Wahofiwa Kufa Katika Ajali ya Ndege Comoro

0
Mfano wa ndege iliyopata ajali

Watu 14 wakiwemo marubani wawili wa Tanzania, wanahofiwa kupoteza maisha baada ya ndege ndogo waliyokuwa wakisafiria kutoka Kisiwa cha Moroni kuelekea Kisiwa cha Moheri, Comoro kupata ajali na kuzama baharini.

 

Kapteni Mazrui Mohamed wa Kampuni ya Fly Zanzibar ambao ndiyo wamiliki wa ndege hiyo, ameeleza kuwa ndege hiyo ilikodishwa wiki moja iliyopita kwenda Comoro na walipata taarifa za kupotea kwa ndege hiyo hapo jana na baada ya kufuatilia katika kifaa maalum cha kufuatilia safari za ndege, waligundua kwamba ilipoteza mawasiliano ikiwa inaelekea katika Kisiwa cha Moheri.

 

Mazrui ameeleza kwamba shughuli za uokoaji zimekuwa ngumu kutokana na hali mbaya ya hewa na tayari baadhi ya mabaki ya ndege hiyo yameonekana katika Pwani ya Moheri ingawa mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyeokolewa.

Leave A Reply