The House of Favourite Newspapers

Waziri Mkuu India Awakubali Kili Paul na Neema

0

Siku chache baada ya Balozi wa India nchini Tanzania, Binaya Pradhan kukutana na vijana wawili wa Kitanzania, Kili Paul na dada yake Neema jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi ameonesha kufurahishwa na ubunifu wa vijana hao na kueleza kuwa angependa kuwafahamu zaidi.

Waziri Mkuu Narendra, ameyasema hayo katika hotuba yake ya Mann Ki Baat na kueleza kuwa ubunifu mkubwa wa kuigilizia (lip sync) nyimbo za Kihindi kisha kuziposti mitandaoni unaofanywa na vijana hao wa Kimaisai, unaonesha ni kwa namna gani wanaupenda na kuuheshimu utamaduni wa Kihindi.

Kili Paul na Neema katika siku za hivi karibuni, wamepata umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi kwa kuigilizia (lip syncing) nyimbo za wasanii mbalimbali hususan kutoka nchini India na wameendelea kuwa gumzo kwenye mitandao ya Tik Tok na Instagram.

Leave A Reply